AJIKUTA KWENYE CHUMBA CHA KUHIFADHIA MAITI


Msichana mwenye umri wa miaka 17 ambaye aliripotiwa kufariki baada ya kushambuliwa na wananchi wenye hasira kali kwa madai ya kuiba ndizi katika mji wa Apac, Uganda, amepatikana akiwa hai katika chumba cha kuhifadhia maiti, saa chache kabla ya uchunguzi wa kifo chake kuanza.

Mwathiriwa huyo ambaye ni mkazi wa Kata ya Matimia katika tarafa ya Arocha, aliripotiwa kupatikana akiwa hai wakati madaktari katika Hospitali ya Apac wakijiandaa kufanya upasuaji baada ya kufariki dunia.

msemaji wa polisi wa mkoa wa Kyoga Kaskazini, Bw Patrick Jimmy Okema, amesema kuwa "Taarifa zilipokelewa kwamba alifariki baada ya kupigwa na kundi la watu wakimtuhumu kwa wizi. Maafisa wetu walizuru eneo la tukio, walirekodi taarifa na kuufikisha mwili wake katika chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali kuu ya Apac,"

Hata hivyo, wakati madaktari hao wakijiandaa kufanya postmortem, waligundua kuwa bado yuko hai, akapelekwa wodini kwenye mashine ya kusaidia maisha na bado yupo kwenye uangalizi maalum.

Mtu mmoja anashikiliwa kutokana na tukio hilo. Aliwaonya walioko mbioni kujisalimisha polisi kabla ya kutafutwa.

Download/Pakua App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

Post a Comment

Previous Post Next Post