Katika jamii zetu kumekuwa na desturi ya baadhi ya watu kuamini kuwa ni vizuri kuwa na mali fiche ambazo hazijulikani na mwenzi (mke au mume), watoto, au hata ndugu wa damu.
Desturi hii imeanza kujengeka zaidi kwa baadhi ya wanaume kuficha au kufanya miradi kwa siri bila kushirikisha familia, hasa wake na watoto. Hali hii imekuwa ikisababisha kupotea kwa mali, hasa pale kunapotokea kifo cha ghafla cha mhusika.
FAIDA ZA KUTOFICHA MALI NA KUSHIRIKISHA FAMILIA
Familia hunufaika na urithi halali
Hupunguza au kuzuia migogoro ya kifamilia na kijamii
Huleta mwendelezo mzuri wa mali kwa vizazi vijavyo
Husaidia kuimarisha uchumi wa familia
HASARA ZA KUFICHA MALI AU KUWEKA MIRADI FICHE
Kwa utafiti mdogo nilioufanya maeneo yangu ya kazi na mtaani, nimebaini kuwa kuna watu wengi, hususan wanaume wanaoishi maeneo ya mijini, wana desturi ya kuwa na miradi ambayo familia zao hazijui. Mfano, mtu hununua kiwanja kwa siri au kujenga nyumba bila familia kufahamu.
Desturi hii ina hasara kubwa, zikiwemo:
Familia kupoteza haki ya kurithi mali halali
Kuongezeka kwa umasikini wa familia kwa sababu hawajui namna uchumi ulivyojengwa
Kusababisha migogoro ya kifamilia
Sote tunasafiri katika dunia hii. Pale tunapopata mali, ni muhimu tujitahidi kuishirikisha familia ili kuepuka madhara yanayoweza kujitokeza pale tunapofariki au kupata matatizo yatakayotuondolea uwezo wa kueleza mali zetu.
IMEANDALIWA NA:
John Francis Haule
Mkuu wa Soko la Samunge
Jiji la Arusha
Simu: 0756 717 987
Barua pepe: haulej46@yahoo.com


Social Plugin