SIMBA SC YAENDELEA KUKICHAFUA NBCPL, YAONDOKA NA USHINDI WA 3-1 DHIDI YA SINGIDA BIG STARSNA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

KLABU ya Simba imeendelea kuuwasha moto kwenye ligi ya NBC hasa kwa kutoa dozi za uhakika kwa timu za ligi hiyo ambapo leo imefanikiwa kuichapa timu ya Singida Big Star kwa mabao 3-1.

Mchezo huo ambao ulipigwa kwenye dimba la Benjamini Mkapa Jijini Dar es Salaam, tumeshuhudia mshambuliaji raia wa Congo Jean Baleke akiweka kambani tena kwa mara nyingine tokea alivyojiunga na miamba hiyoya msimbazi.

Haikuishia hapo tu, nyota wa timu hiyo Saidi Nitbazonkiza nae alifanikiwa kuingia kambani tena kwa kufunga bao la pili kwenye mchezo huo ambalo liliwapeleka mapumziko wakiwa mbele kwa mabao 2-1 huku bao pekee la Singida Big Star likifungwa na Bruno Gomez

Bao la tatu la Simba Sc lilifungwa na Osman Sakho akipokea krosi kutoka kwa Shomari Kapombe, bao ambalo liliwashua mashabiki wengi kwani linataka kufanana na lile ambalo alifunga kwenye michuano ya CAF mwaka jana.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post