MADIWANI SHINYANGA, WAKUU WA DIVISHENI NA VITENGO WAPEWA MAFUNZO YA MAADILI YA VIONGOZI WA UMMA

Madiwani wa Manispaa ya Shinyanga na Wakuu wa Divisheni na Vitengo wakiwa kwenye mafunzo ya maadili ya viongozi wa umma.

Na Marco Maduhu, SHINYANGA

MADIWANI wa Halmashauri ya Manispaa pamoja na Wakuu wa Divisheni na Vitengo, wamepewa mafunzo ya maadili ya viongozi wa umma, ambayo ndiyo nguzo kuu katika utendaji kazi na kusukuma gurudumu la maendeleo kwa wananchi wa Manispaa hiyo.

Mafunzo hayo yametolewa leo Februari 11, 2023 katika ukumbi wa Mikutano wa Manispaa hiyo ya Shinyanga.

Akitoa mafunzo hayo Katibu Msaidizi Ofisi ya Rais Secretariate ya maadili ya viongozi wa umma Kanda ya Magharibi Gerald Mwaitebele, amesema uzingatiaji wa maadili ni muhimu sana kwa viongozi wa umma na kufanya vizuri katika utendaji wao kazi.

“Maadili ni kinga kwa viongozi, na kuna utafiti umefanyika kuwa asilimia 80 ya mafanikio kwa viongozi ni kuzingatia maadili, na maadili hua yanafanya viongozi kuwa waadilifu katika utendaji kazi na kufikia malengo yao,”amesema Mwaitebele.

Aidha, ametaja faida ya maadili kwa viongozi wa umma, kuwa yatawafanya kutoa maamuzi sahihi, kuwa wawajibikaji na wawazi, kufanya kazi kwa pamoja (Teamwork), kupendana, kuheshimiana, na kushauriana namna ya kufanya kazi na kufikia malengo waliyojiwekea.

Katika hatua nyingine ametaka vitendo visivyo vya maadili kwa viongozi wa umma, kuwa ni kutumia madaraka vibaya na kujipatia fedha isivyo halali, kuweka shinikizo ili mtumishi wa umma afukuzwe kazi kinyume cha sheria, na kutumia lugha za matusi.

Ameendelea kutaja vitendo vingine visivyo vya maadili kuwa ni kuegamia upande mmoja wakati wa kutatua migogoro, kupingana kauli hadharani na kiongozi mwingine, kupokea zawadi ya fedha ambayo inazidi Shilingi laki mbili, pamoja na kuwa chanzo cha kuanzisha migogoro badala ya kuwa kimbilio la suluhisho.

Kwa upande wake Meya wa Manispaa ya Shinyanga Elias Masumbuko, amesema mafunzo hayo ya maadili kwa viongozi wa umma yamewagusa, huku akiwataka viongozi, madiwani na watumishi wote wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga wayazingatie na kuwaongoza katika utendaji wao kazi.

Katibu Msaidizi Ofisi ya Rais Secretariate ya maadili ya viongozi wa umma Kanda ya Magharibi Gerald Mwaitebele, akitoa mafunzo ya maadili ya viongozi wa umma kwa Madiwani na Wakuu wa Divisheni na Vitengo Manispaa ya Shinyanga.

Afisa Maadili Secretarite ya maadili ya viongozi wa umma Vupala Mbwilo, akitoa mafunzo ya maadili ya viongozi wa umma kwa Madiwani na Wakuu wa Divisheni na Vitengo Manispaa ya Shinyanga.

Meya wa Manispaa ya Shinyanga Elias Masumbuko (kushoto), akiwa na Naibu Meya Ester Makune (katikati) na Afisa Utumishi Getruda Gisema, kwenye mafunzo ya maadili ya viongozi wa umma.

Meya wa Manispaa ya Shinyanga Elias Masumbuko akiwa kwenye mafunzo ya maadili ya viongozi wa umma.

Meya wa Manispaa ya Shinyanga Elias Masumbuko (kushoto) akiwa na Naibu Meya Ester Makune kwenye mafunzo ya maadili ya viongozi wa umma.

Afisa Utumishi Manispaa ya Shinyanga Getruda Gisema akiwa kwenye mafunzo ya maadili ya viongozi wa umma.

Katibu Tawala wilaya ya Shinyanga Boniphace Chambi (kushoto) akifuatilia mafunzo ya maadili ya viongozi wa umma.

Madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga wakiwa kwenye mafunzo ya maadili ya viongozi wa umma.

Mafunzo ya maadili ya viongozi wa umma yakiendelea.

Watumishi wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga wakiwa kwenye mafunzo ya maadili ya viongozi wa umma.

Afisa elimu shule za Msingi Manispaa ya Shinyanga Neema Mkanga akifuatila mafunzo ya maadili ya viongozi wa umma.

Afisa elimu Sekondari Manispaa ya Shinyanga Lucas Mzungu akifuatilia mafunzo ya maadili ya viongozi wa umma.

Watumishi wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga wakiwa kwenye mafunzo ya maadili ya viongozi wa umma.

Mafunzo ya maadili ya viongozi wa umma yakiendelea.

Mafunzo ya maadili ya viongozi wa umma yakiendelea.

Mafunzo ya maadili ya viongozi wa umma yakiendelea.

Mafunzo ya maadili ya viongozi wa umma yakiendelea.

Mafunzo ya maadili ya viongozi wa umma yakiendelea.

Mafunzo ya maadili ya viongozi wa umma yakiendelea.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments