AMFUMANIA MKEWE MJAMZITO AKIFANYA MAPENZI NA NJEMBA WODINI ALIKOLAZWA


Mwanaume mmoja raia wa Uganda amepigwa na butwaa baada ya kumpata mkewe mjamzito ambaye alikuwa amelazwahospitalini akifanya mapenzi na barobaro wa miaka 24.

Mwanamke huyo alifumaniwa  na mumewe alipokwenda kumjulia hali katika Hospitali ya Apac ambako alikuwa amekaa kwa siku tano kwa sababu ya kuugua malaria.

Alex Okuta, mkazi wa Kijiji cha Abwal “A” katika kaunti ndogo ya Chegere kutoka Wilaya ya Apac alithibitisha kwamba mkewe mgonjwa alimchiti.

 "Nilifanya ziara ya kushtukiza hospitalini kummwangalia mke wangu ndipo nikampata jamaa huyo kitandani na mke wangu mjamzito," alifichua, na kuongeza kuwa mke wake "amelazwa kwa sababu alikuwa anaugua malaria."

Daily Monitor inaripoti kwamba awali, polisi katika Wilaya ya Apac hawakuwa na shtaka la la kumfungulia kijana huyo anayeishi kwa kuchoma nyama katika Jiji la Apac.

 "Tumependekeza mashtaka ya kusababisha kero ya umma dhidi ya mshukiwa, lakini bado tunachunguza na tutawajulisha kwa wakati unaofaa," ilisema ripoti ya Alhamisi, Januari 12,2023.

Mshtakiwa alipenya katika wadi ya wanawake wiki jana na Joseph Onuk, msimamizi wa Hospitali ya Apac, alijutia kisa hicho ambacho anaamini kingeweza kuepukwa mara ya kwanza.

 "Ninamlaumu mume wa mwanamke huyo," alisema.

 “Unawezaje kumpeleka mkeo hospitali na kuchukua muda mrefu bila kuja kumuona? Wanaume wengine kila wakati wanasema kuwa wana shughuli nyingi. Mtu ambaye hana shughuli nyingi atakunyang'anya mkeo," alisema.

Mwaka jana, bado jamaa mwingine alijikuta katika hali ya kizungumkuti mkee alipomfichulia ana mimba ya mwanamume mwingine.

Jamaa huyo aliomba ushauri kutoka kwa watu mitandoani kwani mpenzi alimsihi asimteme akiahidi kumpeleka mtoto huyo kwa babake pindi tu atakapozaliwa.

Kila mmoja wao alikuwa na hisia mseto baadhi wakionesha kuchanganyikiwa huku wengine nao wakionesha imani mambo yatakuiwa sawa.

Chanzo - Tuko News

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post