AMUUA KWA KUMPIGA NGUMI MKEWE BAADA YA KULA MKATE WOTE


Mwanamke mmoja na mama wa watoto watano ameaga dunia akidaiwa kupigwa na mume wake kwa sababu ya mkate.

Hili limetokea eneo la Enugu nchini Nigeria.
 
Mwanamke huyo kwa jina Ogochukwu Anene na mume wake Ndubisi Wilson Uwadiegwu wanaripotiwa kuwa katika ndoa ambayo iliyoandamwa na vita vya nyumbani.


Siku hiyo, mwanamke huyo anasemekana kumuomba mume wake kuinunulia familia mkate lakini akasema kuwa hakuwa na pesa. 

Mwanamke huyo kisha alitumia pesa zake kununulia familia mkate na Mumewe Ndubuisi anaripotiwa kuingia jikoni na kuula mkate wote.

Baada ya kumlalamikia kwa kumaliza mkate wote bila kusaza hata kidogo wa watoto, mumewe anasemekana kumpiga mkewe kwa ngumi pamoja na kioo.

 Alizirai wakati wa kipigo hicho na kuaga dunia saa chache baadaye.

 Wale waliomjua Ogochukwu walikimbia kwenye mtandao wa Facebook wakitaka haki kutendekea huku ripoti zikisema kuwa mumewe alikuwa huru na akipanga kumzika bila kuijulisha ipasavyo familia ya mke wake.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post