MGODI WA ALMASI MWADUI WAWAHAKIKISHIA WAATHIRIKA WA TOPE WOTE KULIPWA FIDIA

 Meneja Mkuu wa Mgodi wa Almasi Mwadui (Williamson Diamond Limited) Mhandisi Ayoub Mwenda akizungumza na Wananchi ambao ni Waathirika wa tope la Mgodi huo wa vijiji viwili vya Ng'wanholo na Nyenze Kata ya Mwadui Luhumbo wilayani Kishapu kwenye Mkutano wa hadhara.

Na Marco Maduhu, KISHAPU

MGODI wa uchimbaji madini ya Almasi (Williamson Diamond Limited) uliopo Mwadui wilayani Kishapu mkoani Shinyanga, umewatoa wasiwasi wananchi ambao ni waathirika wa kubomoka kwa bwawa la mgodi huo la kuhifadhia maji machafu, na kuharibu maeneo yao ikiwamo makazi kufunikwa na tope, kuwa hakuna ambaye hatolipwa fidia.
 
Meneja Mkuu wa Mgodi huo wa Almasi Mhandisi Ayoub Mwenda, amebainisha hayo leo Januari 10,2023 wakati akizungumza na wananchi wa vijiji vya Ng'wanholo na Nyenze Kata ya Mwadui Luhumbo wilayani Kishapu, ambao ni waathirika wa tope la Mgodi, kwenye Mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji cha Ng'wanholo.

Amesema Mgodi huo kwa sasa unasubiri watalaamu wamalize kufanya tathmini, ndipo waanze utaratibu wa kuwalipa fidia waathirika wote, na hakuna mtu ambaye hatalipwa fidia bali wote watapata haki zao kwa mujibu wa sheria.

"Malipo ya fidia yanategemea kukamilika kwa tathmini, hivyo nawaomba wananchi muwe na subira wakati zoezi la tathmini bado linaendelea, na hakuna ambaye hatolipwa fidia bali kila mtu atapata haki anayostahili," amesema Mwenda.

Aidha, amesema tangu tukio hilo la bwawa la mgodi kubomoka Novemba 7 mwaka 2022, licha ya kuendelea na taratibu za tathmini ili wananchi walipwe fidia, pia wameendelea kutoa huduma zote za kibinadamu kwa waathirika ikiwamo chakula, malazi na wanafunzi kuwapatia mahitaji yote ya shule.

Nao wananchi ambao ni waathirika wa tope la mgodi huo akiwemo Elias Mabele mkazi wa kijiji cha Nyenze, na Peter Bundala mkazi wa Ng'wangholo, wamesema tangu litokee janga hilo la bwawa kubomoka, hadi leo hakuna kinachoendelea juu ya kulipwa fidia zao.

Wamesema wamekuwa wakiona watu wanapishana kwenye maeneo yao wakija kuwahoji tangu mwezi Novemba mwaka 2022, lakini hadi sasa Mwezi Januari 2023 bado hawajajua hatima yao na hawana Makazi wala maeneo ya kulima, huku wakishukuru kupewa majibu juu ya hatma ya kulipwa fidia, na kuomba zoezi hilo lifanyika haraka ili wapate haki zao.

Meneja Mkuu wa Mgodi wa Almas Mwadui (Williamson Diamond Limited) Mhandisi Ayoub Mwenda akizungumza na Wananchi ambao ni Waathirika wa tope la Mgodi huo wa vijiji viwili vya Ng'wanholo na NyenzeKata ya Mwadui Luhumbo wilayani Kishapu kwenye Mkutano wa hadhara.

Afisa Mahusiano Mgodi wa Almasi Mwadui (Williamson Diamond Limited) Bernard Mihayo akizungumza na Wananchi ambao ni Waathirika wa tope la Mgodi huo wa vijiji viwili vya Ng'wanholo na NyenzeKata ya Mwadui Luhumbo wilayani Kishapu kwenye Mkutano wa hadhara.

Mwananchi Maimuna Kasala akizungumza kwenye Mkutano huo wa hadhara.

Mwananchi Elias Mabele akizungumza kwenye Mkutano huo wa hadhara.

Meneja Mkuu wa Mgodi wa Almasi Mwadui Mhandisi Ayoub Mwenda (kushoto) akiwa na Afisa Mahusiano wa Mgodi huo Bernard Mihayo kwenye Mkutano huo wa hadhara.

Viongozi mbalimbali wakiwa kwenye Mkutano huo wa hadhara.

Wananchi wa vijiji vya Ng'wanholo na Nyenze Kata ya Mwadui Luhumbo wilayani Kishapu ambao ni Waathirika wa tope la Mgodi wa Mwadui, wakiwa kwenye Mkutano huo wa hadhara.

Wananchi wakiwa kwenye Mkutano wa hadhara.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments