MAJAMBAZI WANNE WADAKWA DAR...NI WALE WANAODAIWA KUPIGA TUKIO KARIAKOO, KAWE, KUNDUCHI NA GOBA


Moja ya tukio walilofanya majambazi hao
Kamanda wa Jeshi la Polisi Kanda maalum ya Dar es Salaam ACP Muliro Jumanne Muliro
 **
Jeshi la Polisi Kanda Maaalum ya Dar es Salaam, linawashilikilia watuhumiwa wawili wa uhalifu wa kutumia silaha kati ya watuhumiwa wanne ambao wanatuhumiwa kufanya matukio ya unyang'anyi kwa kutumia silaha Kariakoo, Goba, Kawe na Kunduchi.

Akizungumza jijini Dar es Salaam Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro, amesema watuhumiwa hao ambao kwa sasa wapo katika hali mbaya baada ya kujeruhiwa na risasi baada ya majibizano ya risai na polisi eneo la Mabibo External wanatuhumiwa kufanya vitendo vya uporaji fedha kwa kutumia silaha aina ya AK 47 ambayo ina usajili kutoka nje ya Tanzania.

Aidha Kamanda Muliro amesema watuhumiwa baada ya kukamatwa na kuhojiwa kabla ya kupelekwa Muhimbili walisalimisha silaha mbili ikiwemo bunduki aina ya AK 47 iliyokutwa na magazine 24 pamoja na bastola ndogo huku pia wakikutwa na pikipiki mbili pamoja na vifaa vingine mbavyo wanadaiwa kuvitumia kwenye uhalifu.

Kwa upande wao baadhi ya wahanga wa matukio ya uhalifu wa kutumia silaha ikiwemo tukio ambalo picha zake zimesambaa mitandaoni linalodaiwa kutokea eneo la Goba wamelishukuru jeshi la polisi kwa kufanikiwa kuwakamata wahalifu hao ambao waliwavamia na kutaka pesa kwa nyakati tofauti huku wakitumia silaha za moto kama bunduki kupora fedha .

Chanzo - EATV

Download/Pakua App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

Post a Comment

Previous Post Next Post