KIJANA AMUUA BABA YAKE KWA KUMKATA PANGA


Polisi katika kaunti ya Busia nchini Kenya wameanzisha msako wa kumsaka kijana mwenye umri wa miaka 22, baada ya kumkatakata baba yake wa kambo, 66, hadi kumuua kutokana na mzozo wa ardhi.

Mshukiwa mtoro aliyetambuliwa kwa jina Kevin Omusolo, anadaiwa kufanya kitendo hicho cha kinyama katika kijiji cha Aciit eneo bunge la Teso Kusini , Jumamosi usiku.

Kwa mujibu wa Citizen Digital, mkuu wa polisi wa Teso Kusini, Stephen Kimunya alithibitisha kisa hicho akisema marehemu, Abisancio Opili, alikuwa na majeraha mabaya mwilini mwake baada ya kucharangwa mapanga.

Kimunya alibaini kuwa chifu wa eneo hilo alitoa ripoti ya mauaji kwa polisi, ambao walifika katika eneo la tukio.

Kimunya alisema maafisa wake waliona majeraha kwenye mwili wa marehemu, na uchunguzi ulibaini kuwa alipigana na mwanawe wa kambo kuhusu kipande cha ardhi kinachozozaniwa na Omusolo.

Mwili wa marehemu ulihamishwa hadi katika hifadhi ya maiti ya hospitali ya kaunti ndogo ya Alupe ili kuhifadhiwa kabla ya uchunguzi kufanywa ili kubaini chanzo cha kifo hicho.

Chanzo: Tuko News

Download/Pakua App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

Post a Comment

Previous Post Next Post