YANGA SC YAJICHIMBIA KILELENI, YAIFUMUA NAMUNGO FC 2-0

NA EMMANUEL MBATILO

KLABU ya Yanga imefanikiwa kuichapa Namungo Fc kwa mabao 2-0, mechi ambayo imepigwa katika dimba la Majaliwa mkoani Lindi.

Mabao ya Yanga yamefungwa na Yannick Bangala dakika 40 na bao la pili likifungwa na Tuisila Kisinda dakika ya 83 ya mchezo.

Ushindi huo wa Yanga sc umewafanya kuwaweka nafasi nzuri ya juu wakiwa na pointi 38 akifuatiwa na Simba mwenye pointi 34.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post