MWANDISHI WA HABARI GWIJI WA MICHEZO AFARIKI QATAR AKIRIPOTI MICHUANO YA KOMBE LA DUNIA


Mwanahabari maarufu wa kandanda kutoka Marekani amefariki dunia alipokuwa akiripoti kuhusu michuano ya Kombe la Dunia nchini Qatar.


Grant Wahl, 48, alianguka ghafla alipokuwa akitazama mchezo wa Argentina na Uholanzi Ijumaa usiku.

Ripoti za awali zinaonyesha alipatwa na "Mshtuko" lakini hii bado haijathibitishwa rasmi.

Mwezi uliopita Bw Wahl alizuiliwa kwa muda mfupi na mamlaka ya Qatar kwa kujaribu kuingia uwanjani akiwa amevalia shati la upinde wa mvua, kuunga mkono haki za wapenzi wa jinsia moja LGBT.

Katika taarifa, Shirikisho la Soka la Marekani lilisema "Limesikitswa sana" na habari hizo. "Mashabiki wa soka na uandishi wa habari wa ubora wa juu zaidi walijua kwamba tunaweza kutegemea Grant kila wakati kutoa hadithi za utambuzi na za kuburudisha kuhusu mchezo wetu, na wahusika wake wakuu," ilisema taarifa hiyo.

Grant alikua akituma ujumbe katika ukurasa wake wa Twitter kuhusu mechi ya Uholanzi na Argentina, kabla taarifa ya kifo chake kutangazwa.
Chanzo - BBC SWAHILI
Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments