TVMC YAADHIMISHA SIKU 16 ZA KUPINGA UKATILI WA KIJINSIA KWA KUTOA ELIMU NSALALA...."WANAOJIGAMBA BAADA YA KUACHIWA BADO TATIZO"


Mkurugenzi wa Shirika la TVMC Shinyanga Mussa Ngangala akizungumza wakati wa maadhimisho ya siku 16 za kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia katika Kata ya Nsalala Halmashauri ya Shinyanga.

Na Shinyanga Press Club Blog

Jamii imetakiwa kuendelea kuwafichuaa watu wanaofanya vitendo vya ukatili wa kijinsia kutokana na kuwa chanzo cha umasikini kwenye familia na kuharibu ndoto za watoto kwa kuwakatisha masomo kutokana na kupata ujauzito katika umri mdogo pamoja na kukomesha ndoa za utotoni.

Akizungumza na wakazi wa Kata ya Nsalala Mkurugenzi wa Shirika la TVMC lenye makao makuu yake Manispaa ya Shinyanga Mussa Ngangala,amesema katika kuadhimisha siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia wameamuaa kuwafikia wananchi vijijini ili kutoa elimu itakayosaidia kukomesha vitendo hivyo ambavyo bado ni changamoto kwenye jamii.

Ngangala amesema kila mtu ana wajibu wa kumlinda mtoto dhidi ya vitendo vya ukatili wa kijinsia na kuhakikisha anakuwa salama wakati wote anapokuwa nyumbani na shuleni,kutokana na vitendo vya ukatili kuisababishia hasara serikali kwa kutumia fedha nyingi kuhudumia madhura wa ukatili.

Kwa upande wa mimba na ndoa za utotoni,Mussa ameiomba jamii kuacha kuwalinda watu wanaoharibu ndoto za watoto wao kwa kuwakatisha masomo baada ya kupata ujauzito,badala yake wawe mstari wa mbele kutoa taarifa kwa viongozi ili wachukuliwe hatua kali za kisheria ili kukomesha matukio hayo.

“Bado tuna changamoto kubwa ya mimba na ndoa za utotoni sasa ni jukumu letu sisi sote kama wazazi kupinga vitendo hivyo ili viweze kukoma na kuwawezesha watoto kufikia ndoto zao, hakikisheni mnafuatilia mienendo ya watoto wenu wanapokuwa nyumbani hasa wakati wa likizo pia kujua changamoto wanazokumbana nazo wanapokwenda shule”, amesema Ngangala.

Nao baadhi ya wakazi wa Kata ya Nsalala Juliana Paul na Kazimili Shuhuli wamesema vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa wanawake na watoto ni tatizo kubwa na kuiomba serikali kupitia kwa Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga kusaidia kukomesha vitendo vya ukatili kwa watoto na kuchukuwa hatua kali.

Wakazi hao wa Nsalala wamesikitishwa na kitendo cha watuhumiwa wa vitendo vya ukatili wa kijinsia wakiwemo wanaowapa mimba wanafunzi kuachiwa huru na kuonekana mitaani wakitoa maneno ya majigambo jambo ambalo wamesema linaongeza machungu kwa madhura wa ukatili kutokana na kukaa muda mfupi na kurejea tena mitaani na kuiomba serikali kuchukua hatua kali za kisheria ili liwe fundisho kwa wengine.
Mkazi wa Kata ya Nsalala Kazimili Shuhuli akitoa maoni yake jinsi ya kukabiliana na vitendo vya ukatili wa kijinsia.
Cloudi Malunde kutoka MC Entertainment akizungumza kwenye maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia Kata ya Nsalala.
Juliana Paul akizungumza kwenye maadhimisho hayo
Mkutano unaendelea
Wananchi wa Nsalala wakifuatilia matukio yaliyokuwa yanaendelea

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments