MHUBIRI AONYA WANAUME KUPIGIA MAGOTI WANAWAKE.... "UKIMKOSEA USIPIGE MAGOTI, MNUNULIE KAKITU"


Mhubiri tatanishi James Ng'ang'a maarufu kama Pasta Ng'ang'a amewashauri wanaume jinsi ya kuishi vizuri na wake zao lakini kupiga magoti si moja ya nasaha zake.


Ng'ang'a amewaonya wanaume dhidi ya kuwapigia magoti wanawake wanapoomba msamaha akisema hicho ni kitendo cha uoga ambayo haifai kuwa sifa ya mwanaume.

Kwa mujibu wa mhubiri huyo, watu hukoseana katika ndoa na wanaume wanapaswa kutumia mbinu mbadala kuomba wake zao msamaha badala ya kuwapigia magoti. 

"Wanaume msiwe mnapiga magoti kwa wanawake hata ukimkosea. Sisi huwa hatupigi magoti kwa wanawake, tunamnunulia kakitu," Pasta Ng'ang'a alisema.

Mchungaji huyo wa kanisa la Neno Evangelism Centre anasema kuwa ni wanawake wanaostahili kuwapigia bwana zao magoti na wala si vinginevyo. 

"Yeye ndio anafaa apige magoti, akuambie samahani. Sisi hatupigi magoti, sisi ndio makomando. Ukitaka mke wako aone umetubu, unamnunulia kitu," Pasta Ng'ang'a aliongeza.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments