BIBI AUAWA KWA KUKATWA MAPANGA SHINYANGA


Bibi aliyefahamika kwa jina la Mbalu Shija (68) mkazi wa kijiji cha Mwalukwa wilayani Shinyanga, ameuawa kwa kukatwa mapanga kichwani na ubongo kutoka nje akidaiwa ni mshirikina.

Tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia leo Desemba 23,2022  majira ya saa 7 usiku akiwa amelala nyumbani kwake.

Mwenyekiti wa kijiji Mwalukwa Lucas Buchambi akisimulia tukio hilo leo, amesema Bibi huyo huwa anaishi na wajukuu zake, lakini usiku huo hawakuwepo walikuwa kwa jirani wakijiandaa maandalizi ya kuimba kwaya kwenye mkesha wa sikukuu ya Krismasi.

Amesema wajukuu zake waliporudi nyumbani usiku huo, ambapo mmoja hua analala na bibi yake alipoingia chumbani akamuona bibi yao ameanguka chini akiwa ameuawa, ndipo akapiga kelele kuomba msaada.

"Baada ya kupata taarifa za tukio hili majira ya saa 8 usiku niliamka nikaenda eneo la tukio na kumkuta bibi huyu akiwa ameuawa vibaya kwa kukatwa mapanga kichwani huku ubongo ukiwa nje," amesema Buchambi.

                   SOMA >>HAPA>> ZAIDI 

                              CHANZO - NIPASHE

Download/Pakua App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

Post a Comment

Previous Post Next Post