WEADO WAFANYA KIKAO NA KAMATI ZA MTAKUWWA SHYDC, MUNISSY AWATAKA WANAUME WAWE NA HOFU YA MUNGU KUBAKA WATOTO WADOGO

Afisa Miradi Shirika la WEADO Winnie Hinaya akizungumza kwenye kikao hicho cha uchechemuzi na Kamati wa MTAKUWWA.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Nice Munissy akizungumza kwenye kikao hicho.

Na Marco Maduhu, SHINYANGA

SHIRIKA la Women Elderly Advocacy and Development Organization (WEADO) limefanya kikao cha uchechemuzi na Kamati za MTAKUWWA Kata za Masengwa, Tinde na Wilaya, wilayani Shinyanga kujadili na kuweka mikakati namna ya kuzuia mimba na ndoa za utotoni.


Kikao hicho kimefanyika leo Desemba 8,2022 katika ukumbi wa mikutano Shule ya Sekondari ya wasichana Tinde, huku Mgeni Rasmi akiwa ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Nice Munisy.

Afisa miradi kutoka Shirika hilo la WEADO Winnie Hinaya, amesema wamefanya kikao hicho ili kujadiliana na kubadilishana uzoefu na Kamati za Mtakuwwa, katika kuendeleza mapambano ya kuzuia ndoa za utotoni.

Amesema mradi huo wa vunja ukimya zuia ndoa za utotoni ni wa miaka miwili ambao utakoma Aprili mwakani,kwa ufadhili wa Shirika la Foundation for Civil Society ambao unatekelezwa katika Kata za Masengwa na Tinde.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Nice Munissy, akizungumza wakati akifungua kikao hicho, amesema Serikali itaendelea kushirikiana na wadau wa maendeleo katika kupambana na matukio ya ukatili wa kijinsia ili yaishe kabisa na jamii kubaki salama.

Amesema katika kuendeleza mapambano hayo ya kupinga ukatili wa kijinsia ikiwamo kutokomeza mimba na ndoa za utotoni, jamii pia inapaswa kuwa na hofu ya mungu, na kuacha kufanya mapenzi na watoto wadogo ambao hawana hisia zozote.

"Ili kumaliza ukatili ndani ya jamii pia tunapaswa kumshirikisha Mungu, haiwezekani Mwanaume mzima una kwenda kumbaka mtoto wa miaka sita ambaye hana hata hisia zozote sasa anapata raha gani silaana tu,"amesema Munissy.

Katika hatua nyingine Munissy, amewataka pia watoto pale wanapoona viashiria vya kufanyiwa vitendo vya ukatili, wasisite kutoa taarifa mapema ili wasaidiwe kabla ya kupata madhara, huku akimpongeza mwanafunzi ambaye amekuwa akitoa taarifa juu ya wenzao kufanyiwa vitendo vya ukatili na amempatia fedha Sh.30,000 kwa ajili ya kununua vifaa vya shule.


Kwa upande wake Mratibu wa Dawati la Jinsia kutoka Polisi Mkoa wa Shinyanga Monica Venance, amewasihi wazazi washirikiana na vyombo vya dola pale zinaporipotiwa kesi za ukatili, na siyo kumalizana kimya kimya na watuhumiwa na kusababisha kesi kufutwa na hatimaye ukatili kuendelea ndani ya jamii.


Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Nice Munissy akizungumza kwenye kikao hicho.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Nice Munissy (kushoto) akimpatia fedha Sh.30,000 Mratibu elimu Kata ya Tinde Vumilia Mauna kwa ajili ya kumpatia Mwanafunzi ambaye amekuwa akitoa taarifa za matukio ya ukatili ambayo wanafanyiwa wanafunzi wenzake, fedha ambazo atakwenda kununua vifaa vya shule.

Afisa Miradi Shirika la WEADO Winnie Hinaya akizungumza kwenye kikao hicho

Afisa ufuatiliaji na Tathimini kutoka Shirika la WEADO John Eddy akizungumza kwenye kikao hicho.

Mratibu wa Dawati la Jinsia kutoka Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga Monica Venance akitoa taarifa za matukio ya ukatili na changamoto zake katika kushughulikia kesi za ukatili.

Afisa Maendeleo ya Jamii Halima Tendega akizungumza kwenye kikao hicho.
Afisa Maendeleo ya Jamii Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Happiness Misael akizungumza kwenye kikao hicho.

Afisa Ustawi wa Jamii Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Rehema Owen akizungumza kwenye kikao hicho.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Nice Munissy, (kushoto) akiwa na Afisa Maendeleo ya Jamii Halmashauri hiyo Happiness Misael kwenye kikao cha Mtakuwwa kilicho itishwa na Shirika la WEADO.

Kikao kikiendelea.

Washiriki wakiendelea na kikao.

Washiriki wakiendelea na kikao.

Washiriki wakiendelea na kikao.

Washiriki wakiendelea na kikao.

Washiriki wakiendelea na kikao.

Washiriki wakiendelea na kikao.

Washiriki wakiendelea na kikao.

Washiriki wakiendelea na kikao.

Washiriki wakiendelea na kikao.

Washiriki wakiendelea na kikao.

Washiriki wakiendelea na kikao.

Washiriki wakiendelea na kikao.

Washiriki wakiendelea na kikao.

Picha ya Pamoja ikipigwa.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments