MTOTO WA MIAKA MITATU ALIWA NA FISI KWIMBA


M toto Emanuel Marco Nyagela mwenye umri wa miaka mitatu mkazi wa Kijiji cha Mwangika kata ya Mwabomba wilayani Kwimba mkoani Mwanza amefariki dunia baada ya kuliwa na fisi wakati akienda kuoga kwenye dimbwi akiwa na wenzake.

Tukio hilo jana Desemba 27 saa 12 jioni kijijini hapo baada ya mtoto huyo kunyakuliwa na Fisi na kutokomea nae kuelekea msituni

Baba wa mtoto huyo aitwaye Marco Nyangela amesema alisikia yowe kutoka kwa wanakijiji wakisema mtoto wake ameliwa na fisi ndipo wakaanza kumsaka mtoto huyo na kuishia kuona damu zikiwa zimetapakaa kuelekea kwenye msitu huo

Hadi kufikia leo Desemba 28/2022 asubuh wamefanikiwa kuona nguo alizokuwa amevaa mtoto huyo, fuvu la kichwa na ubongo pamoja na meno mawili

Germanus Masala ni mwenyekiti wa kijiji hicho na Amede Sosteness àmbae ni diwani wa kata ya Mwabomba wamesema wataendelea kushirikiana na wanakijiji kuwasaka fisi hao huku wakiwataka wazazi kuwa makini na watoto wao hasa nyakati za usiku.

CHANZO - EATV

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments