MVULANA WA MIAKA 11 AJICHIMBIA KABURI KISHA KUJIUA KISA HAJANUNULIWA NGUO MPYA ZA KRISMASI


Mvulana mmoja wa miaka 11 amejiua katika kijiji cha Kibongoti, kaunti ya Kirinyaga nchini Kenya sababu kuu ikiwa babu na nyanyake kuchelewa kumnunulia nguo mpya za sikukuu ya Krismasi.

Akithibitisha kisa hicho, mkuu wa polisi eneo hilo Moses Koskei alisema kuwa uchunguzi katika kifo cha mwanafunzi huyo wa darasa na nne umeanzishwa na maafisa wake.

Koskei alisema kuwa mamaake mwendazake ambaye hufanya kazi nchini Qatar alikuwa ametumia wazazi wake pesa za kumnunulia mjukuu wao nguo mpya.

Hata hivyo nyanya na babu walimtaka mjukuu wao kuwa mvumilivu na kusubiri kupata nguo mpya baada ya Krismasi kwa sababu ya bei ya sasa ya nguo.

“Inakaa alikuwa ameongea na mamaake ambaye alimthibitishia kuwa alikuwa ametuma pesa. Ninadhani alichukulia ombi la subira kutoka kwa nyanya na babu yake kama kukataa kumnunulia nguo mpya,” Koskei alisema.

Nyanyake Rose Ritho alisimulia jinsi mtoto huyo huyo alivyokuwa amechimba shimo refu katika boma hilo kabla ya kisa hicho.

Alipomuuliza mtoto huyo alimwambia kuwa alikuwa anapanga kupanda mgomba wa ndizi katika shimo hilo.

Nyanya alimuonya na kumtaka alizibe akimwelekezea kuwa ni hatari kuwa na mgomba wa ndizi karibu na waya wa umeme.

Chanzo: Tuko News

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments