MWANAFUNZI WA KIDATO CHA KWANZA ALIYEKUTWA AKIANDIKA BARUA YA MAPENZI AJIUA DAR


Na Mwamvua Mwinyi-Pwani

LASMIN KONDO mwanafunzi wa kidato cha kwanza katika shule ya sekondari ya Masaki , wilayani Kisarawe Mkoani Pwani,amekutwa akiwa amejinyonga baada ya kukatazwa na wazazi wake kutojihusisha na mapenzi .

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo, Kamanda wa jeshi la polisi mkoani Pwani ,ACP -PIUS LUTUMO anasema ,ni matukio mawili ya watu wawili kupoteza maisha katika matukio mawili tofauti yaliyotokeza wilayani Kisarawe.

Akielezea tukio la kwanza, alieleza mwanafunzi huyo amejinyonga baada ya kugombezwa na wazazi wake kutojihusisha na matukio ya mapenzi kufuatia kukutwa na barua aliyokuwa amemuandikia mpenzi wake.

Katika hatua nyingine,kamanda LUTUMO ameeleza kuwa PILI MANG’OTA ambaye ni mkulima wa mboga mboga na mkazi wa Sanze Kisarawe ,amekutwa amefariki dunia.

“Mwanamke huyu aliaga kwenda Visegese kuchukua mboga lakini hakurudi tena hadi umauti ulipomkuta na kukutwa vichakani akiwa amefukiwa akiwa amefariki”alifafanua Lutumo.

Kufuatia kifo cha mwanamke huyo, jeshi hilo linamsaka mtu mmoja aliyejulikana kwa jina la ABDALLAH ambae ni mume wa marehemu kwa tuhuma za kuhusika na kifo cha mkewe .

Jeshi hilo pia limeendelea na msako wake na kufanikia kubaini matukio mengine ya uhalifu.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments