BAISKELI CHANZO KIFO CHA MWANDISHI WA HABARI TBC JOACHIM KAPEMBE KWENYE MLIMA KILIMANJARO

 Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) limetoa ufafanuzi juu ya taarifa ya kifo cha Joachim Vicent Kapembe raia wa Tanzania (45) kilichotokea katika Mlima Kilimanjaro.Kupitia taarifa iliyotolewa na Afisa uhifadhi mwandamizi Catherine Mbena imeeleza kuwa Kapembe amefariki dunia jana majira ya saa 12;00 jioni katika kituo cha Kibo (Kibo Hut) kufuatia ajali ya baiskeli aliyokuwa anaiendesha kama sehemu ya utalii.

Kapembe ambaye katika uhai wake alikuwa mtumishi wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) alikuwa mmoja kati ya watu ambao walipanda Mlima Kilimanjaro wakati wa kwenda kuzindua mtandao wa internet katika kilele cha Uhuru.

Mwandishi huyo wa habari alifikwa na umauti wakati wa kushuka kutoka kilele cha Uhuru baada ya kupata ajali ya baiskeli aliyokuwa akiendesha kutoka kituo cha Kibo kuelekea Kituo cha Horombo. Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya KCMC - Moshi.

Aidha TANAPA imetoa pole kwa familia ya marehemu, watumishi wa TBC, wanahabari na Taifa kwa ujumla kwa kupoteza nguvu kazi ya Taifa.

Download/Pakua App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

Post a Comment

Previous Post Next Post