MTUMBWI WAZAMA NA KUUA WATU NANETakribani watu wanane, akiwemo mama na mtoto wake wa miezi miwili, wamefariki baada ya mtumbwi kuzama mtoni katika huko Nimba kaskazini mashariki mwa Liberia mwishoni mwa wiki.

Miili saba kati ya hiyo iliopolewa kutoka mto Yarr na kuzikwa haraka karibu na mto huo, mamlaka za eneo hilo zimesema.

Vikosi vya uokoaji siku ya leovimesema kwamba hawana matumaini ya kuupata mwili wa mtoto huyo.

Mkuu wa wilaya mini humo, Jefferson Saye Gondah, alisema uwezekano wa kuupata mwili wa mtoto huyo ni mdogo.

Waliouawa ni miongoni mwa watu 18 waliokuwa wakirejea kutoka mashambani mwao katika mtumbwi uliochimbwa ambao ulizama katikati ya mto huo. Watu 10 walifanikiwa kuogelea hadi ufukweni

Eatv

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post