WFT - TRUST YAKUTANA NA WADAU KUBADILISHANA UZOEFU MASUALA YA MTAKUWWA AWAMU YA KWANZA, UKATILI WAPUNGUA SHINYANGA

Mratibu wa Mfuko wa Ruzuku wa wanawake Tanzania (WFT-Trust) mkoani Shinyanga Glory Mbia akizungumza kwenye kikao cha kubadilishana uzoefu masuala ya MTAKUWWA awamu ya kwanza.

Na Marco Maduhu, SHINYANGA

MFUKO wa Ruzuku wa wanawake Tanzania (WFT-Trust) umefanya kikao na mashirika ambayo wameyapatia Ruzuku ya kutekeleza mradi wa kupinga ukatili dhidi ya wanawake na watoto, wanabadiliko ngazi ya jamii, pamoja na viongozi kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii Jinsia wanawake na makundi Maalum, kwa lengo la kubadilishana uzoefu juu ya masuala ya Mtakuwwa awamu ya kwanza.

Kikao hicho kimefanyika leo Novemba 1, 2022 katika ukumbi wa mikutano Karena Hotel Mjini Shinyanga.

Mratibu wa Mfuko wa Ruzuku wa wanawake Tanzania (WFT-Trust) mkoani Shinyanga Glory Mbia, amesema wameendesha kikao hicho na mashirika ambayo wanayapatia Ruzuku, wanabadiliko ngazi ya jamii pamoja na viongozi kutoka Wizara ya maendeleo ya jamii jinsia wanawake na makundi Maalumu, kwa ajili ya kubadilishana uzoefu juu ya mpango mkakati wa kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto (MTAKUWWA) awamu ya kwanza ambao umeishia june mwaka huu.

“Mpango Mkakati wa kitaifa wa Serikali wa kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto ulianza mwaka 2017,na umeisha Juni mwaka huu (2022), hivyo ikiwa sisi ni sehemu ya kutekeleza mpango huu tumefanya kikao cha kubadilishana uzoefu na kutoa mapendekezo ya mpango mwingine ujao, kutokana na uzoefu na utafiti tuliofanya” amesema Mbia.

“Katika Mkoa wa Shinyanga tulianza kutoa Ruzuku kwa Mashirika ambayo yanajihusisha na utetezi wa haki za wanawake na watoto mwaka 2020, ili kuunga mkono juhudi za Serikali katika mapambano ya kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto na shughuli hizi zilikuwa zikitekelezwa katika kata 18 halmashauri ya wilaya ya Shinyanga,”ameongeza.

Naye Mkurugenzi mwenza wa Mfuko wa Ruzuku wa wanawake Tanzania (WFT-Trust) Rose Marandu, akizungumza kwenye kikao hicho kwa njia ya mtandao (zoom), amesema wamekuwa wakitoa Ruzuku kwa mashirika hayo kutokana na Mkoa wa Shinyanga kuwa na kiwango kikubwa cha matukio ya ukatili wa wanawake na watoto.

Amesema katika utoaji wa Ruzuku hizo, wameshaanza kuona mafanikio makubwa, ambapo vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto vimeanza kupungua, huku akitoa mapendezo kwa Serikali kuondoa Sera au Sheria ambazo zinakinzana katika utetezi wa haki za wanawake na watoto.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa watoto kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii Jinsia wanawake na Makundi Maalum Sebastian Kitiku, ameipongeza WFT-Trust kwa kazi kubwa ambayo wanaifanya kwa kuyafadhili mashirika na kuifikia jamii kwa ukaribu zaidi na kutoa elimu juu ya madhara ya vitendo vya ukatili.

Pia ameupongeza Mkoa wa Shinyanga kuwa Mkoa wa kwanza katika mapambano ya kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto, ikiwamo kuzindua mpango wake mkakati wa kutokomeza ukatili wa wanawake na watoto na kuwa mkoa wa mfano.

Aidha, amesema kutokana kazi kubwa ambayo wameifanya Mkoa huo waShinyanga kwa kuweka juhudi kubwa katika mapambano ya kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto, ndiyo sababu kubwa ambayo imewafanya kufanya ziara kwa ajili ya kufanya tathimini ya utekelezaji wa Mtakuwwa.

Mratibu wa Mtakuwwa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Aisha Omary, halmashauri ambayo ilikuwa ikitekelezewa mradi wa kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto kwa mashirika ambayo yalipewa Ruzuku na WFT-Trust, amesema ukatili wilayani humo umepungua kwa kiasi kikubwa tofauti na miaka ya nyuma.

Amesema pia kumekuwepo na utoaji wa taarifa za matukio ya ukatili wa kijinsia kwa jamii, pamoja na watoto kutoa taarifa kupitia mabaraza ya watoto na wamefanikiwa kuzui ndoa za utotoni 14, pamoja na kumfunga Jela miaka 30 Mwalimu wa Skauti aliyekuwa akilawiti watoto.

Mratibu wa Mfuko wa Ruzuku wa wanawake Tanzania (WFT-Trust) mkoani Shinyanga Glory Mbia akizungumza kwenye kikao cha kubadilishana uzoefu masuala ya Mtakuwwa awamu ya kwanza.Mratibu wa Mfuko wa Ruzuku wa wanawake Tanzania (WFT-Trust) mkoani Shinyanga Glory Mbia akizungumza kwenye kikao cha kubadilishana uzoefu masuala Mtakuwwa awamu ya kwanza.


Mkurugenzi wa idara sera na mipango kutoka Wizara ya Maendeleo ya jamii jinsia wanawake na makundi maalum Sayi Katwale akizungumza kwenye kikao hicho.

Mkurugenzi wa idara ya watoto kutoka Wizara ya Maendeleo ya jamii jinsia wanawake na makundi maalum Sebastian Kitiku akizungumza kwenye kikao hicho.

Mratibu wa Mtakuwwa kutoka Wizara ya Maendeleo ya jamii jinsia wanawake na makundi maalum Joel Mangi akizungumza kwenye kikao hicho.

Pastory Mfoi akizungumza kwenye kikao hicho kwa niaba ya Mtaribu wa Mtakuwwa Mkoa wa Shinyanga.

Mratibu wa Mtakuwwa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Aisha Omary akizungumza kwenye kikao hicho.

Mkurugenzi wa Shirika la ICS mkoani Shinyanga Kudely Sokoine akizungumza kwenye kikao hicho.

Kikao cha tathimini Mtakuwwa awamu ya kwanza kikiendelea.
Kikao cha tathimini Mtakuwwa awamu ya kwanza kikiendelea.
Kikao cha tathimini Mtakuwwa awamu ya kwanza kikiendelea.
Kikao cha tathimini Mtakuwwa awamu ya kwanza kikiendelea.
Kikao cha tathimini Mtakuwwa awamu ya kwanza kikiendelea.

Kikao cha tathimini Mtakuwwa awamu ya kwanza kikiendelea.

Kikao cha tathimini Mtakuwwa awamu ya kwanza kikiendelea.

Kikao cha tathimini Mtakuwwa awamu ya kwanza kikiendelea.

Kikao cha tathimini Mtakuwwa awamu ya kwanza kikiendelea.

Kikao cha tathmini Mtakuwwa awamu ya kwanza kikiendelea.
Kikao cha tathimini Mtakuwwa awamu ya kwanza kikiendelea.

Kikao cha tathmini Mtakuwwa awamu ya kwanza kikiendelea.
Kikao cha tathmini Mtakuwwa awamu ya kwanza kikiendelea.
Kikao cha tathmini Mtakuwwa awamu ya kwanza kikiendelea.

WFT-Trust kutoka Makao makuu Dar es Salaam wakishiriki kikao kwa njia ya mtandao (zoom).
Picha ya pamoja ikipigwa mara baada ya kumalizika kwa kikao.


Picha ya pamoja ikipigwa mara baada ya kumalizika kwa kikao.

Kwa mawasiliano zaidi kwa WFT Trust, Piga simu +255 753 912 130, tuma barua pepe kwa info@wftrust.or.tz au tembelea tovuti www.wft.or.tz

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post