Mkurugenzi wa Manunuzi Benki ya CRDB, Pendason Philemon (watatu kulia) na Moureen Mollel, Meneja Mipango ya Biashara Benki ya CRDB (wapili kushuto) pamoja na viongozi wengine waandamizi wa benki hiyo katika picha ya pamoja wakionyesha tuzo ya Benki Bora katika kipengele cha Huduma kwa Wateja (Most Preferred Domestic Bank at Customer Service) na tuzo ya Huduma Bora za Kidijitali katika Sekta ya Benki (Most Advanced Digital Banking Services) Afrika Mashariki ambazo benki hiyo imetunukiwa katika hafla ya tuzo za Consumer Choice Awards zilizofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee jana Novemba 12, 2022. Hii ni mara ya pili mfululizo kwa Benki ya CRDB kushindo tuzo hizo zinazotokana na maoni ya wateja/ watumiaji wa huduma.
Mkurugenzi wa Manunuzi Benki ya CRDB, Pendason Philemon (kulia) akipokea tuzo ya Huduma Bora za Kidijitali katika Sekta ya Benki (Most Advanced Digital Banking Services) Afrika Mashariki kutoka kwa Mkurugenzi wa Biashara na Masoko Vodacom, Linda Riwa katika tuzo zako Consumer Choice Awards zilizofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee jana Novemba 12, 2022. Katika tuzo hizo Benki ya CRDB pia ilitunukiwa tuzo ya Benki Bora katika kipengele cha Huduma kwa Wateja (Most Preferred Domestic Bank at Customer Service).
Mkurugenzi wa Manunuzi Benki ya CRDB, Pendason Philemon (kulia) akipokea tuzo ya Benki Bora katika kipengele cha Huduma kwa Wateja (Most Preferred Domestic Bank at Customer Service) kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kilombero Sugar, Guy Williams katika tuzo za Consumer Choice Awards zilizofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee jana Novemba 12, 2022. Katika tuzo hizo Benki ya CRDB pia ilitunukiwa tuzo ya Huduma Bora za Kidijitali katika Sekta ya Benki (Most Advanced Digital Banking Services) Afrika Mashariki.
===== ====== ======
Benki ya CRDB imeendelea kudhihirisha kuwa benki bora na kinara nchini kwa kutunikiwa tuzo mbili za umahiri katika sekta ya fedha nchini katika tuzo za Consumer Choice Awards zilizofanyika jana Novemba 12, 2022 katika ukumbi wa mikutano wa Diamond Jubilee Jijini Dar es Salaam.
Tuzo ilizotunukiwa Benki ya CRDB ni ile ya tuzo za Huduma Bora za Kidijitali Afrika Mashariki, pamoja na Huduma Bora kwa Wateja. Hii ni mara ya pili mfululizo kwa Benki ya CRDB kushindo tuzo hizo zinazotokana na maoni ya wateja/ watumiaji wa huduma.
Akizungumza wakati wa kupokea tuzo hizo, Mkurugenzi wa Manunuzi Benki ya CRDB aliwashukuru wa wateja, washirika, wadau wa benki hiyo, pamoja na Watanzania wote kwa kuendelea kuifanya Benki ya CRDB kuwa bora zaidi.
"Tunawashukuru sana kwa kuendelea kutufanya kuwa bora zaidi. Ahadi yetu ni kuendelea kuwa wabunifu katika huduma zetu ili kusaidia kuboresha maisha ya Watanzania," alisema Pendason.
Katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita, Benki ya CRDB imefanya mageuzi makubwa ya kimkakati katika biashara yake ambayo yamepelekea kupata matokeo mazuri kiutendaji, ikiwa ni pamoja na uboreshaji wa huduma, na ukuaji wa faida.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB amewashukuru wateja, wanahisa na wawekezaji wa Benki hiyo kwa kuifanya benki hiyo kuendelea kuwa bora zaidi.
Mwaka 2022 umekuwa wamafanikio makubwa kwa Benki ya CRDB hivi karibuni benki hiyo inetunukiwa tuzo mbili za ‘Benki Bora Tanzania kwa na majarida maarufu ya fedha na uchumi duniani ya Euromoney na Global Finance kutambua umahiri wake katika kuongeza ujumuishi wa kifedha katika ukanda wa Afrika Mashariki na kuboresha maisha ya watu.
Pendason ameishukuru Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuboresha mazingira ya biashara nchini akibainisha hiyo pia imekuwa chachu ya Benki ya CRDB kufanya vizuri.