MAWAKALA WATANO WAKAMATWA WAKISAJILI LAINI ZA SIMU KWA KUTUMIA NAMBA ZA NIDA ZA WATU WENGINE KAGERA


Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Kagera Bw. John Joseph akizungumza na waandishi wa Habari katika ukumbi wa ofisi za Takukuru leo Novemba 02,2022


***

Na Mbuke Shilagi Kagera.

Mawakala watano wa kusajili laini za simu wamekutana na mkono wa Taasisi ya kupambana na Kuzuia Rushwa (TAKUKURU) Mkoani Kagera kwa kusajilia watu laini za simu kwa kutumia namba za NIDA za watu wengine kinyume cha taratibu na sheria.


Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Kagera Bw. John Joseph leo Novemba 02,2022 katika ukumbi wa ofisi za Takukuru akizungumza na vyombo vya habari wakati akitoa taarifa ya miezi mitatu ya miradi ya maendeleo mbalimbali katika maeneo tofauti ndani ya Mkoa wa Kagera.


Amesema kuwa pamoja na kufanya ufuatiliaji wa miradi ya maendeleo pia wamefuatilia usajili wa laini za simu na kubaini baadhi ya mawakala wa usajili wa laini za simu kutokuwa waadilifu na waaminifu.


Ameongeza kuwa mawakala hao wamekuwa wakisajili laini za simu kwa namba za NIDA za watu wengine na baadhi ya laini hizo kutumika katika uhalifu ambapo vijana watano tayari wamekamatwa na uchunguzi wa kina unaendelea.

Aidha amewataka wananchi wote wa Kagera wanapokwenda kusajili laini zao za simu kuwa makini sana kutokana na namba za simu nyingi zimekuwa na majina tofauti.Aidha amewataka wananchi kwenda kwa mawakala wa simu ili kuangalia namba zao za NIDA zimesajili namba ngapi na Kama itaonekana namba ambazo huzifahamu uweze kuwasiliana na makampuni ya laini husika ili zifungiwe mara moja ili kuepusha usumbufu.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments