TANZANIA INA KILA SABABU YA KUWA MWANACHAMA WA GROUP ON EARTH OBSERVATIONS (GEO)


Na Edwin Soko Accra - Ghana - GEO Reporter

Katika Jiji la Accra  Nchini Ghana kuna mkutano wa.jukwaa la mwaka  2022 la Group on Earth Observations(GEO WEEK 2022).

Takribani Nchi 113 zikiwa ni wanachama wa GEO, kati ya hizo Nchi 30 zinatoka Afrika, kati ya hizo 30 Nchi 4 zinatoka katika ukanda wa Afrika ya Mashiriki, ikiwemo Uganda, Kenya, Rwanda na Congo ambayo imepata uanachama kwenye mkutano wa mwaka huu (GEO 2022) hapa Accra.

Jukwaa hili lina umuhimu mkubwà  kwa kuwa, linawaleta wadau wa Kidunia  pamoja kupitia Serikali zao pamoja taasisi zisizo za kiserikali ili kujadili  umuhimu wa ulimwengu wa kesho kwa kuzingatia maamuzi na mipango  ya leo yenye faida na ustawi wa binadamu kwa kuweka uwiano sawa wa ukuaji wa  teknolojia na utunzaji wa mazingira yenye ustahimilivu.Resilient)

Ndani ya jukwaa hili kuna jukwaa jingine dogo la upande wa Nchi za Afrika linaitwa, AfriGEO, ambapo lengo lake kuu ni  kukuza uelewa wa Earth Obervation, kutengeneza sera za kikanda na ushirikiano miongoni mwa Nchi za Afrika.

Lakini pia kuna mkakati mpana wa kuhakikisha linatafuta rasilimari fedha ili Nchi wanachama wa GEO kutoka Afrika washiriki majadiliano ya kila Mwaka na kuwa majadiliano ya kikanda yenye maudhui ya Afrika zaizi.

Shughuli hizi za AgriGEO ndio zinafanya tafakuri yangu kuwa na hoja ya umuhimu wa  Tanzania kujiunga na jukwaa la GEO la.Dunia na moja kwa moja kuwa katika mjumuiko wa jukwaa dogo la AfriGEO.

Jukwaa  la AfriGEO linasaidia  utengamano wa GEOGLOW  ECMWF kwenye utabiri wa majanga ya asili kwa ushahidi wa kitakwimu.

Jukwaa l la AfriGEO liinaratibu mwenendo wa mazao na hali ya hewa  katika Nchi ya Rwanda, Kenya , Ethiopia na Tanzania licha ya Tanzania kutokuwa mwanachama lakini inanufaika na jukwaa.

Kutengeneza tovuti ya Afrika yenye taarifa, tafiti na kazi  zote za Earth Observations.

Kushirikiana na wadau wengine wa kimataifa juu ya uhifadhi na ufuatiliaji wa uendelevu wa rasilimari asili za Dunia.

Kufanya tafiti za pamoja kati ya wataalamu wa uhifadhi wa Dunia na wataalamu wa afya na kuja na majibu ya changamoto zilizopo.

Kuandaa shindano la wataalamu  GEO  vijana wa toka Nchi mbalimbali za Afrika na kuwapa ruzuku za kuendeleza mawazo bunifu ya kuiweka Dunia katika usalama kwa kutumia takwimu na teknolojia.

Kufanya tafiti za kitakwimu kwa kutumia teknolojia rahisi na kumaliza changamoto za jamii za pembezoni mwa Dunia.

Hizo ni faida chache kwa AfriGEO ambalo ni jukwaa la uratibu wa Nchi za Aftika  lakini kwa jukwaa kuu la kidunia nako kuna faida nyingi ila nitazitaja chache.

Nchi  wanachama zinanufaika  na ruzuku za maandiko miradi yenye kutoa saluhisho ya matatizo ya kijamii na kimazingira kwa  kutumia  teknolojia na takwimu.

Kubadilishana uzoefu wa kimataifa juu ya masuala ya utunzaji na ufuatiliaji wa Dunia na kasi ya teknolojia.

Kupata  taarifa za awali za majanga ya asili kupitia vituo vya ufuatiliaj vya pamoja na utaalamu wa namna ya kupambana na majanga.

Je ni nyanja  zipi  wanachama wa GEO wanayawekea msisitizo?

Maeneo hayo ni kama.ifuatavyo.

 1 Eneo la akili bandia/ GEO artifiacla intellegence

2.Eneo la  afya, /GEO Health

3. Eneo la usalama wa rasilimari /GEO resource security

4. Eneo la  ustahimilivu wa majanga/ GEO disaster resilience 

Hapa ndipo ninapoona umuhimu wa Tanzania kujiunga kwenye jukwaa kwa kuwa, kuna faida nyingi katika maeneo tajwa hapo juu.

Pia kwa kuwa Tanzania imekuwa mstari wa mbele kwenye kujenga ustahimilivu   kimazingira kupitia  teknolojia hii ni fursa kwa Nchi, hivyo tuchangamkie kama wenzetu  Kenya Uganda, Rwanda na Congo walivyochangamkia.

Mmkutano wa GEO WEEK 2022 ulifungliwa na Makamu wa Rais wa Ghana Doktari Mohamudu Bawumia ambaye alisisitiza  Afrika kuongeza nguvu ya kupatikana kwa taarifa kwa kutumia teknolojia ili kuweza kukabiliana ana athari za kimazingira na kujenga ustahimilivu wa changamoto za kijamii.

Pia vyuo vikuu mbalimbali vyenye ubobezi wa sayansi na teknolojia vimeshiriki kwenye kutoa majibu ya tafiti kikiwemo chuo kikuu cha Twente na chuo kikuu cha Nishati na rasilimari asili cha Ghana(UENR)

Pia taasisi za kisayansi kama US GEO, Arc GIS  na SERVIR west Aftica zilihudhuria mkutano uliokuwa na washiriki zaidi ya 1000.

Jukwaa la GEO WEEK lilianza rasmi Mwaka 2016 na Mwaka huu kwa mara ya kwanza limefanyika Afrika katika Nchi ya Ghana .

Kauli mbiu ya GEO WEEK 202W ni Global Action for Local Impact

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post