Live : MIILI YA WATU 19 WALIOFARIKI KWENYE AJALI YA NDEGE YA PRECISION AIR INAAGWA....KIJANA ALIYESAIDIA KUOKOA APEWA SH. MIL 1


Miili ya marehemu waliofariki katika ajali ya ndege ya Shirika la Precision iliyotokea Novemba 6, 2022, ikiwa imewekwa katika eneo maalum kwenye uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba Mkoani Kagera kwa ajili ya kuagwa na kukabidhiwa kwa ndugu wa marehemu katika maombolezo yaliyofanyika kweye uwaja huo Jumatatu 7/11/2022. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akitoa salamu za mwisho kwa miili ya watu waliopata ajali ya ndege ya shirika la Precision , iliyotokea Novemba 6, 2022. Maombolezo hayo yamefanyika katika uwanja wa Kaitaba Bukoba Mkoani Kagera Jumatatu 7/11/2022

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza na waombolezaji waliojitokeza kuaga miili ya watu waliopata ajali katika ndege ya shirika la Precision, iliyotokea Novemba 6, 2022. Maombolezo hayo yamefanyika katika uwanja wa Kaitaba Bukoba Mkoani Kagera Jumatatu 7/11/2022. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Ndege ya Shirika la Precision iliyopata ajali Novemba 6, 2022 ikiwa pembezoni mwa uwanja wa ndege wa Bukoba baada ya kuvutwa kutoka eneo la ajali. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akimpongeza na kumfariji kijana Jackson Majaliwa kwa ushujaa wake wa kuwahi katika eneo ilipotokea ajali ya ndege ya Shirika la Precision na kuwaokoa abiria waliokuwa wameshindwa kutoka ndani ya ndege hiyo. Maombolezo ya kuaga miili ya watu wa ajali hiyo yamefanyika katika uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba Mkoani Kagera 7/11/2022. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akitoa pole kwa ndugu wa Marehemu waliojitokeza katika uwanja wa Kaitaba yalipofanyika maombolezo ya kitaifa ya wahanga wa ajali ya ndege ya shirika la Precision, Ajali hiyo ilitokea Novemba 6, 2022. Maombolezo hayo yamefanyika katika uwanja wa Kaitaba - Bukoba Mkoani Kagera Jumatatu 7/11/2022. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Majeneza yenye miili ya watu 19 waliofariki katika ajali ya ndege ya Precision Air iliyotokea Jumapili Novemba 6, 2022 katika Ziwa Victoria, Bukoba mkoani Kagera.


Kijana aliyefahamika kwa jina la Majaliwa amepewa kiasi cha Shilingi Milioni Moja baada ya kuokoa manusura wa ajali ya Ndege ya Kampuni ya Precious Air iliyotokea mkoani Kagera ambayo ilisababisha vifo vya watu 19.

Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Albert Chalamila ametoa kiasi hicho cha fedha kwa Kijana huyo mbele ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wakati wa zoezi la kuaga miili ya waliofariki dunia kwenye ajali hiyo katika uwanja wa Kaitaba mkoani humo.

Hata hivyo, RC Chalamila ameiomba Serikali kutoa kiasi cha fedha kutoka Mfuko wa Maafa ili kufanikisha mafunzo maalum ya ukoaji kwa Wavuni wa Ziwa Victoria.

Baada ya kupewa fedha hizo (Milioni Moja) Kijana huyo Mvuvi alishindwa kujizuia na kumwaga machozi huku akipewa mkono wa pongezi na Waziri Mkuu Majaliwa kwa ushujaa wake.

Licha ya kufanikisha kuokoa baadhi ya Watu katika ajali hiyo, Kijana huyo alipoteza fahamu akidai kuwa alipigwa na kamba kichwani kwake akiwa katika harakati hiyo uokozi.

Kupitia hotuba yake, RC Chalamila amemuomba Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa kutoa taarifa zaidi kuhusu Abiria waliokwama kusafiri kwenye uwanja wa Ndege wa Kagera baada ya kutokea ajali hiyo Ziwa Victoria.

Fuatilia matukio yanayoendelea hapa
 

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments