TARURA KUONGEZA KASI KUIMARISHA MIUNDOMBINU YA BARABARA

 
Mtendaji Mkuu wa TARURA Mhandisi Victor Seff,wakati akitoa taarifa ya Utekelezaji wa Shughuli zao na mwelekeo wa utekelezaji wa bajeti kwa mwaka wa fedha 2022/2023 


Dotto Kwilasa, DODOMA

WAKALA  wa Barabara  Vijijini na Mijini (TARURA),umeimarisha miudombinu ya barabara za wilaya kutoka asilimia 15 mpaka asilimia 25 huku hali ya mtandao wa barabara za Wilaya  kwa sasa ikiwa ni asilimia 25, sawa na kilomita  34,056 ambayo ni sawa na asilimia 23.6 .

Hayo ameyasema  Oktoba 3,2022 Jijini Dodoma na Mtendaji Mkuu wa TARURA Mhandisi Victor Seff,wakati akitoa taarifa ya Utekelezaji wa Shughuli zao na mwelekeo wa utekelezaji wa bajeti kwa mwaka wa fedha 2022/2023 huku akifafanua kuwa kilomita 48,684.36 sawa na asilimia asilimia 33.7 ina hali ya wastani na Kilomita 61,689.42 ambayo ni asilimia 42.7 una hali mbaya.

“ Takwimu zetu zinaonesha kuwa asilimia 75.67 ya mtandao wa barabara za Wilaya ni za udongo na zinaathirika sana wakati wa misimu ya mvua na kusababisha maeneo mengi kutofikika. “

“ Mipango ya TARURA ni kuhakikisha inaboresha mtandao wa barabara za Wilaya angalau ziweze kupitika misimu yote.”

Aidha Mhandisi Seff amesema  kuwa ili kupunguza gharama katika kukamilisha mirada mbalimbali za ujenzi wataweka kipaumbele katika matumizi ya malighafi zinazopatikana maeneoya kazi.

“Hadi sasa tumejenga madaraja 110 yenye thamani ya Shilingi bilioni 5 ambapo gharama imepungua kwa zaidi ya asilimia 50. Madaraja hayo yamejengwa katika mikoa ya Kigoma 72, Singida 13, Tabora 3, Kilimanjaro 6, Mbeya 2, Arusha 4, Mrorgoro 2 na Iringa 9,”Amebainisha Seff

Mhandisi Victor amesema kuwa tangu kuanzishwa kwa Wakala hiyo na kuanza majukumu yake mnamo Julai 1,2017 na kukamilika tarehe 30 June 2021 jumla ya Shilingi 1,297.79 milioni fedha za ndani zilitumika.

Amesema Katika kipindi hicho jumla ya barabara zenye urefu wa kilometa 24,979.24 zilifanyiwa matengenezo, kilometa 955.35 zilijengwa kwa kiwango cha lami na kilometa 16,857.82 zilijengwa/karabatiwa kwa kiwango cha changarawe. Aidha, jumla ya madaraja 231 (kutoka Madaraja 2,960 hadi 3,191) na Makalvati 1,325 yamejengwa (kutoka Makalvati 67,992 hadi 69,317)

Katika kipindi hicho jumla ya barabara zenye urefu wa kilometa 24,979.24 zilifanyiwa matengenezo, kilometa 955.35 zilijengwa kwa kiwango cha lami na kilometa 16,857.82 zilijengwa/karabatiwa kwa kiwango cha changarawe ambapo jumla ya madaraja 231 (kutoka Madaraja 2,960 hadi 3,191) na Makalvati 1,325 yamejengwa (kutoka Makalvati 67,992 hadi 69,317).

Amesema mpango mkakati wa pili wa TARURA wa 2021 mpaka 2026 umepanga Kuondoa vikwazo kwenye mtandao wa barabara za Wilaya ili ziweze kupitika misimu yote,Kupandisha hadhi (upgrading) barabara za udongo kuwa za Changarawe/Lami kwa kuzingatia vipaumbele vya kiuchumi na kijamii ikiwa ni pamoja na kupunguza msongamano wa magari katika majiji, manispaa na miji.

Mhandisi Victor Seff ameongeza kuwa kuanzia mwaka 2021/22 hadi 2026/27 lengo la TARURA ni kuwa mtandao wa barabara za lami utaongezeka kwa km 1,450.75 (kilometa 2,404.90 – 3,855.65), changarawe km 73,241.57 (kilometa 29,116.57 – 102,358.14) na madaraja 3,808 (toka 2,812 hadi 6,620) ambapo fedha zitakazotumika kwenye mpango huu zinakadiriwa kuwa Zaidi ya Shilingi trilioni 4.2.

“Lengo la Mpango Mkakati wetu wa pili ni kuwa ifikapo 2025/26 asilimia 85 ya mtandao wa barabara za Wilaya chini ya TARURA zitakuwa zinapitika kwa misimu yote na nyakati za mvua hapatakuwa na taharuki inayojitokeza sasa kwa maeneo mengi kutofikika,”Amesema Mhandisi Seff

Mhandisi seff amesema kwa Mwaka wa fedha 2022/23 ni mwaka wa pili wa utekelezaji wa Mpango Mkakati wa pili ambapo TARURA imetengewa bajeti ya jumla ya Shilingi bilioni 838.16 ambapo kati ya hizo Shilingi bilioni 776.63 ni fedha za ndani na Shilingi bilioni 61.53 ni fedha za nje.

Naye Msemaji wa Serikali na Mkurugenzi wa Idara ya Habari-MAELEZO, Gerson Msingwa amesema katika kipindi cha miaka miwili, Serikali imezipelekea TARURA na Tanroadh kiasi cha Sh trilioni 4.7 kwa ajili ya kujenga na kukarabati miundombinu ya barabara.



Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments