TAAnet KUENDELEA KUPIGANIA UANZISHWAJI SERA NA MIONGOZO YA POMBE NCHINI

 
Katibu Mtendaji Mtendaji wa TAAnet Gladness Munuo.

Na Dotto Kwilasa,DODOMA 

KATIBU Mtendaji wa 
Mtandao wa wadau wanaopambana na unywaji pombe kupita kiasi(TAAnet),Gladness Munuo ameiomba Serikali kudhibiti matumizi ya pombe kupita kiasi kwa kukubali  kuhuisha sera na miongozo ya uuzaji wake.

Katika taarifa yake aliyoitoa kwa vyombo vya habari hivi karibuni katika kuadhimisha siku ya kupinga matumizi ya pombe kupita kiasi (NOALCOHOLDAY)ambayo huadhimishwa kila mwaka ifikapo Oktoba 3 ya Kila mwaka alisema  sheria zilizopo zinapuuzwa kwa kiasi kikubwa hali inayopelekea watu kuendelea kuendesha biashara ya pombe bila  kufuata sheria wala kujali madhara yatokanayo na pombe.
 
Amesema kutokana na hali hiyo takribani watu milioni tatu Duniani kote wameripotiwa kupoteza maisha kila mwaka  kutokana na unywaji wa pombe hivyo Taanet kuona haja ya kuishauri Serikali kulitafutia ufumbuzi tatizo hilo kwa  ubunifu ambao utaokoa maisha, kama vile kutokomeza athari zitokanazo na pombe na unywaji pombe kupindukia. 

Amesema kwa takwimu hizo upo uhusiano ulio dhahiri kati ya matumizi mabaya ya pombe na madhara yanayosababisha magonjwa ya Afya ya Akili, ugonjwa wa Afya ya Akili, tabia zisizoeleweka pamoja na ongezekop la magonjwa yasiyo ambukiza.

"Matumizi ya pombe na athari zake ni tatizo linalozidi kukua nchini Tanzania, na linapaswa kudhibitiwa kwa haraka iwezekanavyo hasa wakati huu ambapo kuna aina nyingi za vilevi vyenye kileo asilimia kubwa ambapo aina hii ya pombe inaenda kuharibu akili za raia na hasa vijana ambao ni tegemeo la nguvu kazi ya Taifa nchini,"amesema na kuongeza,;

Ni dhahiri kabisa kuwa zipo nchi ambazo tayari wameshachukua hatua stahiki ikiwepo Kenya, Uganda, Malawi, Zambia , South Afrika na Burundi ambazo wana Sera za kudhubiti matumizi mabaya ya pombe na tayari matokeo chanya kwa Jamii na Taifa yanaonekana"amesema.

Munuo ameeleza kuwa mbali na matatizo ya kiafya, matumizi ya pombe kupita kiasi madhara makubwa mengine katika Jamii ni ongezeko la ukatili wa kijinsia na kuyumba kiuchumi kunako sababishwa na matumizi ya pombe na utengengezaji wa pombe kupita kiasi.

"Matumizi ya pombe kupita kiasi husababisha vifo vya mapema na ulemavu , Vijana kati ya umri wa miaka 20-39 sawa na asilimia 13.5 vifo vingi husababishwa na unywaji pombe kupita kiasi,"amesema.

Aidha amesema kuwa taarifa hiyo imebainisha kwa asilimia kubwa kuwa upo uhusiano ulio dhahiri kati ya matumizi mabaya ya pombe na madhara yanayosababisha magonjwa ya Afya ya Akili, ugonjwa wa Afya ya Akili, tabia zisizoeleweka pamoja na ongezeko la magonjwa yasiyo ambukiza.

"Matumizi ya pombe na athari zake ni tatizo linalozidi kukua nchini Tanzania, na linapaswa kudhibitiwa kwa haraka iwezekanavyo hasa wakati huu ambapo kuna aina nyingi za vilevi vyenye kileo asilimia kubwa ambapo aina hii ya pombe inaenda kuharibu akili za raia na hasa vijana ambao ni tegemeo la nguvu kazi ya Taifa nchini,"ameeleza Munuo.

Amesema TAAnet imekuwa ikitoa elimu kwa umma juu ya madhara ya unywaji pombe kupita kiasi ambapo Jamii imekuwa ikisumbuka na magonjwa mbalimbali yanayoletelezwa na matumizi ya pombe kupita kiasi kama vile maradhi ya moyo, ini na saratani.

"Tunayo imani kubwa kwa kuwa mikakati ya kuwa na Sera ya Afya yenye kuweka katazo la matumizi mabaya ya pombe itazingatiwa,ikiwa pamoja na kuwepo kwa muongozo wa kudhibiti utengenezaji wa pombe,usambazaji na matumizi ya kinywaji chochote kile chenye kilevi nchini utapewa kipaumbele.

Pia Munuo ameeleza kuwa kwa  mujibu wa utafiti uliofanywa na Shirika la Kimataifa IOGT-NTO Movement, mwaka 2021 walifanya utafiti kuangalia kiwango cha matumizi ya kinywaji cha pombe kwa Jamii kupitia mashirika ya kijamii yanayofadhiliwa na shirika hilo. 

Wakati huo huo amebainisha kuwa wanaume asilimia 51 hunywa pombe na ni kiasi cha zaidi ya mara tatu kwa wiki ambapo Utafiti huo ulidhihirisha kuwa haijalishi ni pombe ya aina gani.

 Mikoa ambayo Utafiti huo ulifanyika ni  Dodoma katika kata ya Iyumbu na Makulu, Mkoa wa Manyara katika wilaya ya Mbulu kata ya Dongobesh na Sanubara, Mkoa wa Iringa, Iringa Vijijini kata za Ifunda ,Kalengakatika na Mkoa wa Arusha maeneo ya Arusha mjini kata ya Ngarenaro na Mkoa wa Kilimanjaro kata za Rombo na Tarakea. 

"Utafiti huu uliwafikia baadhi ya Wabunge wa Bunge la Tanzania ambao ni ‘champions’ wa kutetea matumizi sahihi ya unywaji pombe kwa Jamii na ndiyo vinara wa kuitaka serikali iridhie uwepo wa muongozo wa kudhibiti unywaji, na utengenezaji wa pombe kupita kiasi,"amefafanua Munuo


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post