MAZISHI YA MFANYABIASHARA NA MWEKEZAJI HILAL HAMAD MAARUFU 'PHANTOM' YAFANYIKA MJINI SHINYANGA

 

Mazishi ya aliyekuwa Mfanyabiashara na mwekezaji mzawa wa  mkoa wa Shinyanga HilLal Hamad  maarufu kwa jina la Phantom, yamefanyika leo Jumanne tarehe 04,10,2022, kwenye makaburi ya Waislamu yaliyopo Nguzonane katika Manispaa ya Shinyanga.

Mazishi ya Mwekezaji huyo ambaye pia alikuwa ni kada wa Chama cha Mapinduzi CCM, yamehudhuriwa na watu wa mbalimbali wakiwemo  Wafanyabiashara ,Viongozi wa Serikali, na vyama vya siasa.

Akimzungumzia  msiba huo, Mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM Taifa (NEC) Bwana Gasper Kileo , amesema  marehemu Hillal ameacha pengo kubwa  katika sekta ya uwekezaji na kwenye chama cha Mapinduzi na atakumbukwa kutokana na michango mbalimbali ya hali na mali aliyoitoa.

SAUTI YA GAKI

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Mtaa wa Mabambasi uliopo Kata ya Ndembezi katika Mnispaa ya Shinyanga ambapo alikuwa akiishi Bwana Hillal  enzi za uhai wake  Bakari Khamis Juma, amemwelezea marehemu kuwa, licha ya kuwa na mwekezaji na mfanyabiashara mkubwa,  alikuwa na mahusiano mazuri na jamii anayomzunguka ikiwemo kuchangia shughuli za maendeleo.

Bwana Hillal ambaye amewekeza katika sekta mbalimbali ikiwemo ya mafuta, uchimbaji wa madini na elimu, amefariki dunia jana mchana jijini Dar es salaam, ambako alikuwa akipatiwa matibabu.


Chanzo- Radio Faraja

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post