DC MBONEKO AKEMEA WAZAZI KUWARUBUNI WANAFUNZI WAKIKE WAFANYE VIBAYA MITIHANI YAO YA DARASA LA SABA ILI KUWAOZESHA NDOA ZA UTOTONIMkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko akizungumza na wananchi wa kijiji cha Mwandutu Kata ya Solwa wilayani Shinyanga na kukemea wazazi kutowarubuni wanafunzi wa kike kufanya vibaya mitihani yao kesho ya kuhitimu darasa la saba kwa lengo la kuwaozesha ndoa za utotoni.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko akizungumza na wananchi wa kijiji cha Mwandutu Kata ya Solwa wilayani Shinyanga na kukemea wazazi kutowarubuni wanafunzi wa kike kufanya vibaya mitihani yao ya kuhitimu darasa la saba kwa lengo la kuwaozesha ndoa za utotoni.

Na Marco Maduhu, SHINYANGA

MKUU wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, amekemea vitendo vya baadhi ya wazazi wilayani humo, kuwarubuni watoto wao wa kike ili wafanye vibaya mitihani yao ya kuhitimu darasa la saba kwa lengo la kuwaozesha ndoa za utotoni na kupata mali.

Mboneko amebainisha hayo leo Oktoba 4, 2022 wakati akizungumza na wananchi wa kijiji cha Mwandutu Kata ya Solwa wilayani Shinyanga, alipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya utekelezaji wa mradi wa maji kijijini humo.

Amesema kesho Oktoba 5,2022 wanafunzi wa darasa la saba wanaanza mitihani yao ya kuhitimu elimu ya msingi, na kukemea vitendo vya baadhi ya wazazi ambao wamekuwa na tabia ya kuwaambia watoto wao wa kike wafanye vibaya mitihani yao ili wafeli, na kutumia fursa hiyo kuwaozesha ndoa za utotoni.

“Katika wilaya yangu nataka watoto wote wafaulu mitihani yao ya kuhitimu elimu ya msingi, ili waendelee na masomo ya juu na kutimiza ndoto zao, nawasihi wazazi waacheni watoto wasome watakuja kuwasaidia baadae, msiwarubuni wafanye vibaya mitihani yao ya kuhitimu darasa la saba,”amesema Mboneko.

Aidha, amesema hata kama wakihitimu masomo yao hakuna kuwaozesha ndoa za utotoni bali wawaache wasubiri matokeo yao, na kubainisha kuwa mzazi atakayebainika kuozesha mtoto Serikali itamchukulia hatua kali za kisheria.

“Rais Samia amekuwa akitoa fedha nyingi ili kuboresha miundombinu ya elimu na hivi karibuni ametoa fedha nyingine za kujenga vyumba vya madarasa kwa shule za Sekondari akitaka watoto wasome na kutimiza ndoto zao, hivyo nawaomba wazazi tusimwangushe Rais wetu acheni watoto wasome tena elimu ni bure hadi kidato cha Sita,”amesema Mboneko

Katika hatua nyingine Mboneko, amewataka wananchi watunze akiba ya chakula walichonacho na kuacha kukiuza hovyo, ili kukabiliana na baa la njaa hapo baadae kutokana na hali ya hewa siyo nzuri, pamoja na wakulima kuendelea kujiorodhesha majina yao ili wapate Ruzuku ya Mbolea.

Wananchi wa kijiji cha Mwandutu Kata ya Solwa wilayani Shinyanga wakiwa kwenye Mkutano wa Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post