RAIS SAMIA ATEUA WAKILI MKUU WA SERIKALI NA NAIBU WAKE


Dkt. Boniphace Christopher Luhende, Wakili Mkuu wa Serikali Mteule
**

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania , Mhe. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa Wakili Mkuu wa Serikali na Naibu wakili Mkuu wa Serikali kama ifuatavyo:

Amemteua Dkt. Boniphace Christopher Luhende kuwa Wakili Mkuu wa Serikali, Kabla ya uteuzi huu Luhende alikuwa Naibu Wakili Mkuu wa Serikali,Dkt. Luhende anachukua nafasi ya Bwana Gabriel Paschal Malata ambaye aliteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama Kuu.

Bi. Sarah Duncan Mwaipopo, Naibu Wakili Mkuu wa Serikali Mteule

Amemteua Bi. Sarah Duncan Mwaipopo kuwa Naibu Wakili Mkuu wa Serikali, Kabla ya uteuzi huu Bi. Mwaipopo alikuwa Wakili wa Serikali Mkuu katika Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Bi. Mwaipopo anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Dkt. Luhende ambaye ameteuliwa kuwa Wakili Mkuu wa Serikali.

Uteuzi huu umeanza tarehe 09 Oktoba, 2022.Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post