MAWAZIRI WA UTALII KUTOKA NCHI ZAIDI YA 50 WAKUTANA JIJINI ARUSHA KUWEKA MIKAKATI MIPYA YA KUENDELEZA SEKTA HIYO

 


Na Woinde Shizza , ARUSHA

Waziri Mkuu wa Tanzania Kasim Majaliwa amesema kuwa serikali inaendelea kufanya kila linalowezekana kuimarisha sekta ya utalii hapa nchini .

Aliyasema hayo wakati akifungua Mkutano unaoshirikisha pia wataalam na watafiti wa masuala ya utalii duniani unaofanyika wakati ambapo nchi mbalimbali duniani ambazo uchumi wake unategemea utalii ikiwemo Tanzania bado zinafanya jitihada kubwa kuimarisha sekta za utalii baada ya kuathiriwa kwa kiasi kikubwa na Covid- 19.

Katika Mkutano huo Mawaziri wa utalii kutoka zaidi ya nchi 50 wanachama wa shirika la utalii Duniani na maafisa wa Kamisheni ya  wamekutana jijini Arusha kujadili hali ya utalii ilivyo baada ya athari ya Janga la Covid 19 na pia kuweka mikakati mipya ya kuendeleza sekta hiyo.


Alisema kuwa Mwaka 2019 kabla ya mlipuko wa janga la Uviko 19 mapato yatokanayo na sekta ya utalii nchini Tanzania yalifikia dola za kimarekani Bilioni 2.9 na kuzalisha ajira za moja kwa moja na zisizokuwa za moja kwa moja milioni 2.5

"Na katika kipindi hicho sekta ya utalii ilichangia wastani wa asilimia 17.2 ya pato ghafi la taifa," aliongeza.

Aidha waziri Mkuu aliwaeleza washiriki wa mkutano huo kuwa Tanzania inaendelea kuongeza nguvu katika kulinda na kuhifadhi utalii wa rasilimali za asili na kuhakikisha unaendelea kuwanufaisha wananchi wa nchi hiyo na taifa kwa ujumla

"Hatua hii ni kielelezo tosha cha matokeo ya ushirikiano uliopo kati ya Tanzania na Jumuiya za kimataifa ikiwemo shirika la utali duniania hasa katika kuendelea sekta muhimu ya Utalii pamoja na masuala ya uhifadhi," alisema.

Kwa upande wake katibu wa shirika la utalii Duniani kamisheni ya Afrika  Zurab Pololikashvili alisema pamoja na changamoto zilizopo bado kuna umuhimu wa kuendelea na utalii na akaipongeza Tanzania kwa kuendelea kuimarisha misingi ya uhifadhi na utalii.

"Nafurahi na kufarijika kufika Tanzania kwa mara ya kwanza, nchi ambayo inasifika kwa kitovu cha utali duniania ,baada ya janga la Uviko 19 wakati sasa umefika wa kuinu sekta hii na kuhakikisha inasaidia masuala ya kiuchumi na kijamii," alisema.

Shirika la utalii duniani ambalo kwa sasa makao yake makuu yako Uhispania lilianzishwa mwaka 1946 mjini London, nchini Uingereza na Tanzania ilijiunga na shirika hilo mwaka 1975.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post