YANGA UNBEATEN!! WAENDELEZA UBABE WAKIICHAPA GEITA GOLD 1-0


Na Odilo Bolgas,MZALENDO BLOGS

MABINGWA wa Ligi kuu ya NBC Tanzania bara timu ya Yanga imeendeleza rekodi yao ya kutofungwa katika mechi 45 za ligi baada ya kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Geita Gold mchezo uliopigwa uwanja wa CCM Kirumba, jijini Mwanza.Shujaa wa Yanga ni Winga mtukutu Bernard Morrison aliipatia bao timu yake mnamo dakika ya 45 kwa mkwaju wa penalti baada ya beki wa Geita kuunawa Mpira ndani ya 18.

Kwa ushindi huo Yanga wamefikisha Pointi 20 na kuendelea kukaa kileleni mwa msimamo wa Ligi hiyo.

Mchezo mwingine umepigiwa uwanja wa Sokoine jijini Mbeya Tanzania Prisons imenusurika kufungwa na Namungo FC baada kulazimishwa sare ya kufungana bao 1-1

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post