MATREKTA CHANZO CHA AJALI-ARUSHA



Na Abel Paul wa Jeshi la Polisi

Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha Mrakibu wa Polisi SP SOLOMON MWANGAMILO amewataka madereva na wamiliki wa matrekta katika Mkoa wa Arusha kufuata sheria za usalama Barabarani ili kupunguza ajali ama kumaliza ajali katika Mkoa huo.


SP Solomon Mwangamilo amesema hayo leo Oktoba 20,2022 alipokuwa akizungumza na Madereva na wamiliki wa Matrekta katika kata ya Kikatiti wilaya ya Arumeru Mkoa Arusha ambapo amebainisha kuwa takwimu zinaonyesha kuwa ajali nyingi zinasabibishwa na vyombo hivyo kwa kukosa viakisi mwanga(reflectors).


Aidha SP Solomon Mwangamilo ametoa muda wa mwezi mmoja kufanya ukarabati wa vyombo hivyo nakuweka viakisi mwanga (reflectors) ili kupunguza ajali ambazo zina gharimu Maisha ya watu.


Amesema kuwa baada ya muda huo waliopewa wamiliki wa MaTrekta hayo hakutakuwa na msamaha kwa wamiliki na madereva wa vyombo hivyo.

Nao baadhi ya madereva na wamiliki wa vyombo hivyo wamesema semina na maelekezo waliyoyapata wameyapokea ambapo wamebainisha kuwa hapo mwanzo walikuwa hawana uelewa juu ya madhara ya kutoweka viaksi mwanga katika vyombo vyao.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments