MAKOMBE ACHAGULIWA KWA KISHINDO MWENYEKITI MPYA WA CCM SHINYANGA MJINI


Mwenyekiti mpya wa CCM wilaya ya Shinyanga Mjini Magile Anold Makombe akiwa katika ukumbi wa CCM Mkoa wa Shinyanga kwenye Mkutano Maalumu wa Uchaguzi wa Nafasi ya Uenyekiti CCM wilaya uliofanyika Jumamosi Oktoba 1,2022 kabla ya matokeo kutangazwa
Wagombea watatu wa nafasi ya Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Shinyanga Mjini wakiwa katika ukumbi wa CCM Mkoa wa Shinyanga kwenye Mkutano Maalumu wa Uchaguzi wa Nafasi ya Uenyekiti CCM wilaya uliofanyika Jumamosi Oktoba 1,2022. Kushoto ni Mokhe Warioba Nassor, Pendo John Sawa (katikati) na Magile Anold Makombe (kulia).


**
Wajumbe wa Mkutano Maalumu wa Uchaguzi wa Nafasi ya Uenyekiti CCM wilaya ya Shinyanga wamemchagua kwa kishindo Magile Anold Makombe kuwa Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini.

Katika uchaguzi huo uliofanyika leo Jumamosi Oktoba 1,2022 katika ukumbi wa CCM Mkoa wa Shinyanga Magile Anold Makombe amepata kura 296 akifuatiwa na  Mokhe Warioba Nassor aliyepata kura 144 na Pendo John Sawa akipata kura 74.

Makombe anachukua nafasi ya aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Shinyanga Mjini, Abubakar GulamHafiz Mukadam.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post