WANAWAKE WABAKWA KICHAWI GEITA..."ALIVYO NINANILIU SIKUMUONA SURA"

Wananchi wa Kijiji cha Bugando, Kata ya Nzera, wilayani Geita mkoani humo, wameiomba serikali ichunguze na kumtafuta mtu anayewaingilia usiku wananchi kwenye nyumba zao na kuwabaka hali inayopelekea kuishi kwa mashaka na kuhatarisha afya zao.


Wakizungunza na EATV waathirika wa tukio hilo wanasema mtu huyo amekuwa akiingia kwenye nyumba zao na kuwaingilia kimwili kwa nguvu na baadae anaondoka bila kuchukua kitu chochote kwenye nyumba zao.

"Yaani anakuja kwa mazingira ya kawaida anaingia tu yeye mwenyewe sikumuona sura aliponanilia akawa ameiwasha simu yake alipoiwasha simu akaniambia usinitazame, nikamwambia sasa wewe nani, akaniambia haupaswi kujua, kwanza akaniuliza una watoto, baadae alipomaliza kunaniliu hivyo akawa ameondoka, kwakweli sikubahatisha hata kumuona, ndio hivyo akawa amenibaka," amesema mmoja wa waliobakwa kishirikina.

Diwani wa Viti Maalum wa Kata hiyo Victoria Ndaki, amesema wameanza kufanya vikao kwa ajili ya kuwatambua wanaofanya vitendo hivyo japo Jeshi limezuia kutokana na sababu za kiusalama.

Mkuu wa wilaya ya Geita Wilson Shimo ameiagiza serikali ya Kata kwa kushirikiana na serikali kuu kuanza uchunguzi ili kuweza kuwabaini watu wanaofanya vitendo hivyo.

"Nimeona akina mama hao na kuongea na viongozi wa hapa Nzera na wameshuhudia kwamba haya matendo yanaendelea hapahapa Nzera, vitendo ambavyo sio vya kiungwana na si vya kiutu, tunaanza kufuatilia kwa ukaribu zaidi mienendo na tabia ya watu wanaofanya vitendo hivyo," amesema DC Shimo.

CHANZO - EATV

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post