MREMBO AKAMATWA AKIMTEMBEZEA KICHAPO MUME WAKE


Mwanamke mwenye umri wa miaka 23, ametiwa mbaroni baada ya kudaiwa kumshambulia na kumjeruhi mumewe mtaani Buruburu, Nairobi nchini Kenya.

Ripoti za polisi zilibainisha kwamba Shantel Mutheu mwenye umri wa miaka 33, alimpiga Kitutu Kennedy Oshuka baada ya kutofautiana nyumbani kuhusu bili zilizokosa kulipwa.

Makabiliano yao yaliwavutia majirani waliowasikia wakipigana, na kumukoa Oshuka aliyekuwa akitiririkwa na damu.

 "Jirani aliwaambia polisi kuwa walisikia kelele kutoka kwa nyumba nambari 11 ambayo ni ya Kennedy mwenye umri wa miaka 33.

 Alikimbia hadi kwenye eneo la tukio na kukuta wawili hao wakipigana huku Oshuka akitokwa na damu," sehemu ya ripoti ya polisi kama ilivyonukuliwa na K24 Digital ilisoma.

Mwathiriwa alikimbizwa katika Hospitali ya Mama Lucy Kibaki, ambako amelazwa akiwa mahututi.

 Mshukiwa anazuiliwa na polisi huku uchunguzi kuhusiana na kisa hicho ukiendelea.

 Uchunguzi mwingine hata hivyo ulibainisha kwamba, mwanamke huyo alipandwa na mori, baada ya kugundua kwamba mpenzi wake hakuwa amelipa bili na kuanza kuvunja madirisha.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post