WEADO WATAMBULISHA MRADI WA VUNJA UKIMYA, ZUIA NDOA NA MIMBA ZA UTOTONI WILAYANI SHINYANGA



Mkurugenzi wa Shirika la WEADO Eliasenya Nnko akizungumza wakati wa kutambulisha mradi wa vunja ukimya, zuia ndoa na mimba za utotoni wilayani Shinyanga ambao utatekelezwa Kata ya Masengwa na Tinde wilayani Shinyanga.

Na Marco Maduhu, SHINYANGA

SHIRIKA la Women Elderly Advocacy and Development Organization (WEADO) la Mkoani Shinyanga, limetambulisha mradi wa vunja ukimya, zuia ndoa na mimba za utotoni wilayani Shinyanga.
Mradi huo umetambulishwa leo Oktoba 6, 2022 katika Kata ya Tinde wilayani Shinyanga kwenye ukumbi wa Shule ya Sekondari ya wasichana Tinde (Tindegirls).

Afisa mradi kutoka Shirika la WEADO Winnie Hinaya, akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa mradi huo, amesema utatekelezwa katika Kata mbili Masengwa na Tinde wilayani Shinyanga ndani ya miezi nane ambao utekelezaji wake ni kuanzia Septemba mwaka huu hadi Aprili 2023 kwa ufadhili wa Shirika la Foundation For Civil Society wenye thamani ya Sh.milioni 37.8.

“Lengo la mradi huu ni kupunguza kiwango cha mimba na ndoa za utotoni,”amesema Hinaya.

Aidha, amesema Shughuli ambao zitakuwa zikitumika kwenye mradi huo ni kutoa elimu ya kupinga masuala ya mila na desturi Kandamizi, elimu ya malezi bora, makuzi ya mtoto, mafunzo ya ulinzi na haki za watoto,”ameongeza.

Amesema Kata hizo Masengwa na Tinde wamezipelekea mradi huo kwa kutaka ziwe mfano wa kuigwa katika mapambano ya kumaliza tatizo la mimba na ndoa za utotoni mkoani Shinyanga.

Naye Mkurugenzi wa Shirika la WEADO Eliasenya Nnko, amesema malengo ya mradi huo ni kuona jamii inakuwa salama na hakuna tena mimba wala ndoa za utotoni pamoja na watoto kusoma na kutimiza ndoto zao.

Kwa upande Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Nicodemas Simoni ambaye pia ni diwani wa Masengwa akifungua kikao hicho. amelipongeza Shirika hilo la WEADO kwa mradi huo ambao utasaidia kuokoa ndoto za wanafunzi, huku akiahidi Halmashauri itaendelea kutoa ushirikiano kwa mashirika yote ambayo yanaisaidia jamii.

Aidha, Afisa Maendeleo ya Jamii halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Aisha Omary, amesema wadau wa maendeleo wamekuwa na mchango mkubwa katika mapambano ya kutokomeza mimba na ndoa za utotoni, ambapo katika halmashauri hiyo matukio hayo yamepungua kwa kiasi kikubwa tofauti na miaka ya nyuma, kuwa ndoa za utotoni zilikuwa zikifungwa Tisa hadi 10 lakini sasa zinakomea mbili hadi tatu na zote zinatibuliwa.

Afisa Ustawi wa Jamii Mkoa wa Shinyanga Lidya Kwesigabo, ameitaka jamii wanapozuia mimba na ndoa za utotoni wawakumbuke na watoto wenye ulemavu ambapo wamekuwa wakisahauriwa na kuishia kupewa ujauzito na kuharibu maisha yao.
Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Nicodemas Simon na diwani wa Masengwa akizungumza kwenye utambulisho wa mradi wa Shirika la WEADO.

Mkurugenzi wa Shirika la WEADO Eliasenya Nnko akizungumza wakati wa kutambulisha mradi wa vunja ukimya, zuia ndoa na mimba za utotoni wilayani Shinyanga ambao utatekelezwa Kata ya Masengwa na Tinde wilayani Shinyanga.

Afisa mradi kutoka Shirika hilo la WEADO Winnie Hinaya, akiwasilisha utekelezaji wa mradi huo.
Afisa mradi kutoka Shirika hilo la WEADO Winnie Hinaya, akiwasilisha utekelezaji wa mradi huoAfisa ufuatiliaji na tathimini kutoka WEADO John Eddy akizungumza kwenye utambulisho wa mradi huo.

Afisa Ustawi wa Jamii Mkoa wa Shinyanga Lidya Kwesigabo akizungumza kwenye utambulisho wa mradi huo.

Afisa Maendeleo ya jamii halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Aisha Omary akizungumza kwenye utambulisho wa mradi huo.

Viongozi mbalimbali wa Kata ya Tinde na Masengwa wakiwa kwenye utambulisho wa mradi huo wakiwamo watendaji wa vijiji Kata, Maofisa Elimu, Maendeleo , viongozi wa dini, wazee maarufu, wanafunzi na madiwani.

Kikao cha utambulisho wa mradi kikiendelea.

Kikao cha utambulisho wa mradi kikiendelea.

Kikao cha utambulisho wa mradi kikiendelea.

Kikao cha utambulisho wa mradi kikiendelea.

Kikao cha utambulisho wa mradi kikiendelea.

Kikao cha utambulisho wa mradi kikiendelea.

Wajumbe wakiwa kwenye makundi ya kupanga mpango kazi.

Picha ya pamoja ikipigwa.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments