TBS YATOA USHAURI KWA WAKANDARASI


Afisa Viwango kutoka Shirika Viwango Tanzania (TBS) Innocent Johnbosco akizungumza na Waandishi wa Habari katika banda la Shirika hilo wakati wa maadhimisho ya 19 ya siku ya Wahandisi yanayofanyika jijini Dodoma.

..................................

Na Alex Sonna _DODOMA

WAKANDARASI wameshauriwa kutumia bidhaa zilizothibitishwa ubora wake na Shirika la Viwango Tanzania (TBS) ili kulinda ubora wa kile wanachotengeneza.

Ushauri huo umetolewa leo Septemba 23,2022 na Afisa Viwango kutoka Shirika Viwango Tanzania (TBS)Innocent Johnbosco akizungumza na Waandishi wa Habari katika banda la Shirika hilo wakati wa maadhimisho ya 19 ya siku ya Wahandisi inayofanyika jijini Dodoma.

Johnbosco amesema katika siku ya Wahandisi Tanzania TBS wameshiriki kuendelea kuwahamasisha Wahandisi katika kutoa elimu juu ya viwango vinavyohusiana na project mbalimbali.

"Pia tunaendelea kuhamasisha Wakandarasi kuzalisha na kutumia bidhaa zilizothibitishwa na TBS,"amesema Johnbosco.

Amesema wanaendelea kuwahamasisha wajasiriamali wadogo wadogo waweze kupata nembo za ubora na zinazokidhi viwango ili kumlinda mlaji na kuimarisha uchumi wa Nchi.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post