RAIS SAMIA ATANGAZA SIKU TANO ZA MAOMBOLEZO KUFUATIA KIFO CHA MALKIA ELIZABETH IIKufuatia kifo cha Malkia wa Uingereza, Elizabeth II Septemba 08,2022 nchini Uskochi, Rais wa Tanzania Samia, ametangaza siku tano za maombolezo ya kitaifa kilichotokea September 08,2022 nchini Uskochi.


Maombolezo hayo yataanza September 10,2022 hadi Septemba 14,2022, katika kipindi chote cha maombolezo, bendera zote zitapepea nusu mlingoti nchini Tanzania zikiwemo kwenye Balozi za Tanzania.

Katika taarifa ya Ikulu ya Tanzania imeeleza kuwa Rais Samia amewaomba Watanzania wote kuungana na wenzetu wa Uingereza katika kipindi hiki kigumu cha kuondokewa na aliyekuwa Kiongozi wao nchini humo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post