RAIA WA UGANDA ADAKWA NA MIHURI YA BANDIA YA OFISI ZA SERIKALI AKITUMIA KUFANYIA UHUNI

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Kagera ACP William Mwangaghale akionesha mihuri hiyo
Mihuri iliyokamatwa 

Na Mbuke Shilagi - Malunde 1 blog Kagera.

Jeshi la Polisi Mkoani Kagera linamshikilia mtuhumiwa mmoja raia wa Nchini Uganda kwa tuhuma za kumiliki mihuri idhaniwayo kuwa bandia ya ofisi za Serikali na anayodaiwa kuitumia  katika shughuli zake kwa kugonga kwenye nyaraka mbalimbali kuonyesha kuwa nyaraka hizo zimeidhinishwa na idara husika.

Akizungumza na vyombo vya habari ofisini kwake leo Septemba 06,2022 Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Kagera ACP William Mwampaghale amesema kuwa mtuhumiwa huyo ni mkazi wa Mtukula ambapo amepatikana na mihuri mitatu ya ofisi za Serikali na amekuwa akitumia mihuri hiyo katika shughuli zake kwa kugonga kwenye nyaraka mbalimbali kuonyesha kuwa nyaraka hizo zimeidhinishwa na idara husika.


Ameongeza kuwa walifanikiwa kumkamata mtuhumiwa huyo mnamo tarehe 01 Septemba 2022, katika kitongoji cha Katebe Kijiji Cha Mtukula Wilayani Missenyi akiwa na mihuri mitatu ambapo mmoja ulikuwa muhuri wa Ofisi ya Mamlaka ya Mapata TRA na wa pili ni Muhuri wa ofisi ya Kilimo na watatu ni Muhuri wa ofisi ya Mionzi TAEC.


Aidha mtuhumiwa huyo amekiri kuitumia mihuri hiyo kwa kutengeneza nyaraka ambazo huzitumia kuvusha magari ya mizigo mbalimbali kwenda Nchini Uganda na kwamba mpaka kukamatwa tayari alikuwa kavusha magari ya aina ya fuso tisa na semi trailler mbili.

ACP Mwampaghale amesema kuwa Jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi ili kubaini mtandao wote wa uhalifu wanaojihusisha na uharifu hususani maeneo yote ya mipakani na kuwataka wananchi kuelewa kuwa swala la ulinzi na usalama ni la kila mwananchi.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post