MAITI YAPOTEA MOCHWARI, NDUGU WAAMBIWA WACHUKUE TU MWILI MWINGINE


Familia moja katika kaunti ya Makueni  nchini Kenya imelazimika kuahirisha hafla ya mazishi ya jamaa wao baada ya madai ya kutoweka kwa maiti.

Kulingana na familia ya Waema Nguku, 95, mwili waliopewa na Hospitali ya Rufaa ya Makueni, haukuwa sawa.

Wanasema walikuwa tayari wamenunua jeneza la mzee huyo na kuelekea makafani Alhamisi, Septemba 15,2022 kuchukua mwili wake. Mzee huyo alikuwa anapangiwa kuzikwa Jumamosi, Septemba 17, na matayarisho yalikuwa yamekamilika na hata kaburi lake kuchimbwa, The Standard linaripoti.

Hata hivyo, kizaazaa kilizuka wakati mwili wa mzee huyo ulikosekana kwenye hifadhi ya maiti ya Hospitali ya Rufaa ya Makueni. 

Waliporejea Ijumaa kufuatilia suala hilo, mmoja wa viongozi wa hospitali hiyo aliwaomba kuchukuwa mwili mwingine. 

"Baada ya kushindwa kutonyesha mwili wa baba yetu, tuliondoka na kurejea Ijumaa kufuatilia. Mmoja wa wasimamizi wa hospitali hiyo alituambia tuchukuwe mwili mwingine lakini tulikataa," alisema kifunga mimba wa mzee huyo, Kamene Waema.

Moja ya familia zilizozika jamaa wao wiki jana, imethibitisha kuwa ilipewa mwili usiokuwa sawa na kuutambua kama wa Mzee Nguku. Kufuatia ripoti hiyo, familia ya Nguku sasa inasubiri ripoti ya Idara ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai(DCI). 

Msimamizi wa Hospitali ya Rufaa ya Makueni, Joseph Masila alisema suala hilo linachunguzwa kutambua ni familia ipi ilipewa mwili usiokuwa sawa.

 Rekodi za hospitali hiyo zinaonyesha kuwa miili 12 ilichukuliwa kwa mazishi wiki jana ambapo tano ilikuwa ya wanaume.

 Via TUKO NEWS

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments