MVUA YAUA WATU 300 NIGERIA


Mamlaka nchini Nigeria zinasema kwamba zaidi ya watu 300 wamepoteza maisha huku wengine zaidi ya 100,000 wakiwa hawana mahali pa kuishi kutokana na mafuriko makubwa nchini humo tangu mwezi Julai mwaka huu.

Makazi ya watu na mashamba vimeharibiwa vibaya katika Taifa hilo la Magharibi mwa Afrika ambalo limekumbana na janga baya kabisa la mafuriko kuwahi kutokea kwa miaka mingi iliyopita.

Mamlaka zinasema kwamba majimbo 29 kati ya 36 yameathiriwa vibaya na mafuriko hayo ambayo yamesababishwa na mvua kali zilizoisababisha mabwawa makubwa kufurika na kupelekea maji kufika mpaka nchi jiani ya Cameroon.

Mito pia na yenyewe imefurika maji mengi. Kitengo cha dharura nchini humo kimeonya kwamba marufiko zaidi yanatarajiwa kutokea ndani ya siku zijazo. Serikali imetakiwa kuwaondoa watu kutoka kwenye maeneo ambayo yapo hatarini kukubwa na mafuriko hayo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments