KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YAHIMIZA VIWANDA KUFUATA SHERIA YA UHIFADHI WA MAZINGIRA

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Hamisi Hamza akimuuliza jambo mtaalamu wa kuendesha mashine ya kuyatibu maji taka ambayo yametumika katika kiwanda mara baada ya Kamati ya Kudumu ya Bunge la Viwanda, Biashara na Mazingira kufanya ziara ya kutembelea kiwanda cha shelys kinachotengeneza dawa za binadamu leo Septemba 29,2022 Jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge la Viwanda, Biashara na Mazingira Mhe.David Kihenzile (mwenye shati jeupe) akiwa pamoja na kamati yake wakimsikiliza Msimamizi wa Uzalishaji wa kiwanda cha Shelys kinachotengeneza dawa za binadamu ambapo kamati hiyo ilipofanya ziara ya kutembelea kiwanda hicho leo Septemba 29,2022 Jijini Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge la Viwanda, Biashara na Mazingira Mhe.David Kihenzile (mwenye shati jeupe) akiwa pamoja na kamati yake walipofanya ziara ya kutembelea kiwanda cha Shelys kinachotengeneza dawa za binadamu Jijini Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge la Viwanda, Biashara na Mazingira Mhe.David Kihenzile (mwenye shati jeupe) akiwa pamoja na kamati yake wakimsikiliza Msimamizi wa Uzalishaji wa kiwanda cha Shelys kinachotengeneza dawa ambapo kamati hiyo ilipofanya ziara ya kutembelea kiwanda hicho leo Septemba 29,2022 Jijini Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge la Viwanda, Biashara na Mazingira Mhe.David Kihenzile (mwenye shati jeupe) akiwa pamoja na Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Hamisi Hamza wakitazama mfumo wa kuyatibu majitka baada ya kutumika kwenye kiwanda cha Shelys kinachotengeneza dawa za binadamu ambapo kamati hiyo ilipofanya ziara ya kutembelea kiwanda hicho leo Septemba 29,2022 Jijini Dar es Salaam.

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge la Viwanda, Biashara na Mazingira Mhe.David Kihenzile akipanda mti mara baada ya kufanya ziara ya kutembelea kiwanda cha Shelys kinachotengeneza dawa za binadamu leo Septemba 29,2022 Jijini Dar es SalaamNaibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Hamisi Hamza akipanda mti mara baada ya Kamati ya Kudumu ya Bunge la Viwanda, Biashara na Mazingira kufanya ziara ya kutembelea kiwanda cha Shelys kinachotengeneza dawa za binadamu leo Septemba 29,2022 Jijini Dar es Salaam Mwenyekiti wa Bodi ya Nane ya Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamzi wa Mazingira (NEMC), Prof. Esnati Chaggu akipanda mti mara baada ya Kamati ya Kudumu ya Bunge la Viwanda, Biashara na Mazingira kufanya ziara ya kutembelea kiwanda cha Shelys kinachotengeneza dawa za binadamu leo Septemba 29,2022 Jijini Dar es Salaam Baadhi ya taka ngumu zimehifadhiwa sehemu maalumu kwenye kiwanda cha shelys kinachotengeneza dawa za binadamu kilichopo Jijini Dar es Salaam.

*******************

KAMATI ya Kudumu ya Bunge Viwanda, Biashara na Mazingira imeitaka Serikali kuvichukulia hatua za kisheria Viwanda vyote vinavyotekeleza shughuli zake bila kufuata taratibu za kimazingira.

Agizo hilo limetolewa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe.David Kihenzile mara baada ya ziara ya kamati hiyo kukitembelea kiwanda kinachozalisha dawa mbalimbali za binadamu cha Shelys Pharmaceutical kilichopo Mwenge.

Akiwa kiwandani hapo pamoja na wajumbe wa kamati hiyo, akiwemo Naibu Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe.Khamis Hamza ,Mhe. Kihenzile alisema lengo la hatua hiyo pamoja na mambo mengine ni kulinda afya za wananchi pamoja na viumbe hai.

"Tunapongeza utunzaji na uhifadhi wa mazingira katika kiwanda hiki, ukweli wanafanya kazi nzuri kwa kuyaweka mazingira katika hali ya usafi kuanzia uhifadhi taka hadi mifumo ya mahi ya viwandani, huu ni mfano wa kuigwa" alisema Kihenzile

Alisema suala la kutunza mazingira hasa kwa maeneo ya viwanda ni muhimu kwa kuwa litasaidia kulinda afya za wananchi wa maeneo ya karibu badala ya kuwasababishia maradhi.

Katika hatua nyingine Mwenyekiti huyo wa Kamati ya Viwanda, Biashara na Viwanda ameitaka Ofisi hiyo ya Makamu wa Rais Mazingira kutoa elimu kwa wananchi juu ya utengenishaji wa taka ili kutoa urahisi kwa wasafirishaji wa taka hizo kwenda dampo.

Kwa upande wake Naibu Waziri kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Khamis Hamza alisema wao kama Serikali watahakikisha suala la ukaguzi katika maeneo ya viwanda wanalipa umuhimu ili kulinda aina yoyote ya uhalibifu wa mazingira unaoweza kujitokeza.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments