GO4WASTE, MoCU WAADHIMISHA SIKU YA KIMATAIFA YA KUHAMASISHA UELEWA WA UPOTEVU NA UTUPAJI WA CHAKULA



Mlezi wa Taasisi ya GO4WASTE Anthony Gikuri ambaye pia ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi Tawi la Kizumbi (Moshi Cooperative University - MoCU) na Mjumbe wa Timu ya Afrika ya kuzuia upotevu na utupwaji wa chakula, akitoa elimu ya matumizi sahihi ya chakula kwa vitendo wanafunzi wa Sheer Bliss.

Bango la maadhimisho ya kitaifa ya kuhamasisha uelewa wa upotevu na utupaji wa chakula.

Na Marco Maduhu, SHINYANGA

TAASISI ya GO4WASTE Tanzania kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi Tawi la Kizumbi (Moshi Cooperative University - MoCU)  wameadhimisha siku ya kimataifa ya kuhamasisha uelewa wa upotevu na utupaji wa chakula kwa wanafunzi wa shule ya Sheer Bliss na Chuo cha Ualimu Shinyanga (SHYCOM).

Maadhimisho hayo yamefanyika leo Septemba 29, 2022 na kutolewa elimu kwa njia ya vitendo namna ya uandaaji wa chakula hadi ulaji wake bila ya kusababisha mabaki ya chakula na hatimaye kukitupa.

Mwenyekiti wa Taasisi ya GO4WASTE Tanzania Magreth Nchagwa amesema wamefanya maadhimisho hayo kwa wanafunzi, ambao wanaamini watakuwa mabalozi wazuri wa kwenda kusambaza elimu hiyo na hatimaye kuzuia upotevu na utupwaji wa chakula.

“Leo ni siku ya kimataifa ya kuhamasisha uelewa wa upotevu na utupwaji wa chakula, ambapo tasisi yetu tumeamua kutoa elimu ya matumizi ya chakula kwa vitendo kwa wanafunzi hawa ambao watakwenda kusambaza elimu hii na kufikia watu wengi,”amesema Nchagwa.

Aidha, amesema utoaji wa elimu hiyo pia ndani ya miezi mitatu wanatarajia kufikia vijana zaidi ya elfu 50, kwa kuwatembelea mashuleni na kutumia mitandao ya kijamii.

Naye Mlezi wa Taasisi hiyo, Anthony Gikuri ambaye pia ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi Tawi la Kizumbi (Moshi Cooperative University - MoCU)  na Mjumbe wa timu ya Afrika ya kuzuia upotevu na utupwaji wa chakula  amesema wananchi wamekuwa wakipoteza chakula kingi kwa sababu ya matumizi mabaya.

Nao wanafunzi waliopewa elimu hiyo, kwa nyakati tofauti wameshukuru kupewa elimu namna ya matumizi sahihi ya chakula, ili kuzuia upotevu na utupwaji wa chakula hovyo.

Kauli mbiu ya siku ya kimataifa ya kuhamasisha uelewa wa upotevu na utupwaji wa chakula mwaka huu inasema “Zuia upotevu na utupwaji wa chakula jali watu jali sayari”.

Mlezi wa Taasisi ya GO4WASTE Anthony Gikuri ambaye pia ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi Tawi la Kizumbi (Moshi Cooperative University - MoCU)  na Mjumbe wa Timu ya Afrika ya kuzuia upotevu na utupwaji wa chakula akitoa elimu ya matumizi sahihi ya chakula kwa wanafunzi wa Sheerbliss, kulia ni Mwenyekiti wa Taasisis hiyo Magreth Nchagwa.

Mlezi wa Taasisi ya GO4WASTE Anthony Gikuri ambaye pia ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi Tawi la Kizumbi (Moshi Cooperative University - MoCU)  na Mjumbe wa Timu ya Afrika ya kuzuia upotevu na utupwaji wa chakula, akitoa elimu ya matumizi sahihi ya chakula kwa wanafunzi wa Sheer Bliss.

Mwenyekiti wa Taasisi ya GO4WASTE Magreth Nchagwa, akitoa elimu ya matumizi sahihi ya chakula kwa wanafunzi wa Sheerbliss ili kuzuia upotevu na utupwaji wa chakula.

Mlezi wa Taasisi ya GO4WASTE Anthony Gikuri ambaye pia ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi Tawi la Kizumbi (Moshi Cooperative University - MoCU) na Mjumbe wa Timu ya Afrika ya kuzuia upotevu na utupwaji wa chakula, akitoa elimu ya matumizi sahihi ya chakula kwa vitendo wanafunzi wa Sheer Bliss.

Elimu ya matumizi sahihi ya chakula ikiendelea kutolewa kwa wanafunzi wa Chuo cha Ualimu SHYCOM ili kuzuia upotevu na utupwaji wa chakula hovyo.

Elimu ikitolewa namna ya mtu anavyotaka kula chakula kingi lakini hawezi kukimaliza na hatimaye kusababisha uharibifu wa chakula na kwenda kutupwa.

Chakula kikitupwa mara baada ya mtu kushindwa kukimaliza na kusababisha uharibifu wa chakula.

Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi Tawi la Kizumbi 
(Moshi Cooperative University - MoCU) Denis Silayo akitoa elimu ya matumizi sahihi ya chakula kwa wanafunzi wa Chuo cha Ualimu SHYCOM.

Mhadhiri wa 
Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi Tawi la Kizumbi (Moshi Cooperative University - MoCU) Mustapha Bhoke akitoa elimu ya matumizi sahihi ya chakula kwa wanafunzi wa Chuo cha Ualimu SHYCOM.

Wanafunzi wa chuo cha Ualimu SHYCOM wakiwa katika mafunzo ya matumizi sahihi ya chakula ili kutosababisha upotevu na utupwaji wa chakula.

Wanafunzi wa chuo cha Ualimu SHYCOM wakiwa katika mafunzo ya matumizi sahihi ya chakula ili kutosababisha upotevu na utupwaji wa chakula.

Picha ya pamoja ikipigwa na wanafunzi wa Sheer Bliss.

Picha ya pamoja ikipigwa na wanafunzi wa chuo cha Ualimu SHYCOM.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments