AJIUA KISA KANYIMWA TENDO LA NDOA NA MKEWE


Polisi katika kijiji cha Ebungaya, kaunti ya Kakamega wanachunguza kisa ambapo mwanamume mwenye umri wa miaka 50, anadaiwa kukatiza maisha yake baada ya mzozo wa kinyumbani mnamo Jumatatu, Septemba 5,2022.

Mwili wa Ezra Skim ulipatikana ukininginia kwenye mti ukiwa na kamba shingoni mnamo Jumanne, Septemba 6,2022. 

Marehemu anaripotiwa kutoweka nyumbani kwake mnamo Jumatatu, Septemba 5, kabla ya mwili wake kupatikana na wapita njia.

 Akithibitisha kisa hicho, Afisa Mkuu wa Polisi wa Khayega, Elizabeth Kagehi aliomba kutafuta njia bora ya kusuluhisha migogoro yao badala ya kujitoa uhai.

Akizungumza na waandishi wa habari, dada yake marehemu Jetina Tegeno alisema kaka yake amekuwa akilalamikia kudhulumiwa katika ndoa kabla ya kifo chake. 

Alisema mke wake marehemu amekuwa akimtesa kaka yake na kumyima haki zake za ndoa kila mara.

 "Katika siku zake za mwisho, yeye (Skim) alionekana kuwa na msongo wa mawazo. Amekuwa akimtuhumu mke wake kwa kumdhulumu," Tegeno alisema.

 Akisimulia matukio hayo, mke wake mwendazake Maximila Anyika, alisema walikuwa wamelala wakati Skim kutoka nje ya nyumba bila kurejea.

 "Ghafla alitoka kitandani tulipokuwa tumelala, bila maelezo alitoka nje na kugonga mlango nyuma yake. Tulishtuka kukuta mwili wake ukining'inia kwenye mti," Anyika alisimulia. 

Mwili wa marehemu ulipelekwa katika hifadhi ya maiti ya Mukumu ukisubiri kufanyiwa uchunguzi.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post