RAIS SAMIA ATOA POLE KWA MZEE MWINYI


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Mama Samia Suluhu Hassan (kushoto) akisalimiana na Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Ali Hassan Mwinyi (kulia) alipofika kutoa pole kwa kufiwa na Mtoto wake Marehemu Hassan Ali Hassan Mwinyi, Chukwani Nje ya Jiji la Zanzibar, Mkoa MJini Magharibi (katikati) Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi (kulia kwa Rais) Mbunge wa Fuoni Mhe. Abass Ali Hassan Mwinyi,marehemu Hassan amezikwa Mangapwani Wilaya ya kaskazini “B” Unguja.[Picha na Ikulu]  
Baadhi ya Wanafamilia na Watoto wa Marehemu Hassan Ali Hassan Mwinyi Mtoto wa Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Ali Hassan Mwinyi wakiitikia dua iliyoombwa nyumbani kwao Chukwani Wilaya ya Magharibi “B“ Nje ya Jiji la Zanzibar,wakati Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Mama Samia Suluhu Hassan (hayupo pichani) alipofika kutoa pole kwa msiba walioupata. [Picha na Ikulu] 01/09/2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Mama Samia Suluhu Hassan (wa pili kulia) Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Ali Hassan Mwinyi na Mkewe Mama Siti Mwinyi (katikati) Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi (kushoto) wakiitikia dua iliyoombwa na Sheikh Asumani Mohamed Jengo (kulia) nyumbani kwa Marehemu Hassan Ali Hassan Mwinyi Chukwani Wilaya ya Magharibi “B“ Nje ya Jiji la Zanzibar.[Picha na Ikulu] 01/09/2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Mama Samia Suluhu Hassan (wa pili kulia) Mke wa Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Ali Hassan Mwinyi na Mkewe Mama Siti Mwinyi (kulia) Kizuka wa Marehemu Hassan Ali Hassan Mwinyi Bi,Fauzia Salim Hilal (wa pili kushoto) Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi (kushoto) wakiitikia dua iliyoombwa nyumbani kwa Marehemu Hassan Ali Hassan Mwinyi Chukwani Wilaya ya Magharibi “B“ Nje ya Jiji la Zanzibar.[Picha na Ikulu]

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post