MAMA ALIYETELEKEZEWA MTOTO MLEMAVU NA MUME WAKE ZAIDI YA MIAKA 20 AELEZEA MACHUNGU ANAYOYAPITIA

 

 


Binti mmoja mwenye umri wa 21  anayejulikana kwa jina la Rehema Musa  mkazi wa  Mtaa wa Ilindi Kata ya Zongomera wilayani Kahama Mkoani Shinyanga ambaye ni mlemavu wa viungo vya mwili anapitia changamoto nyingi baada ya kutelekezwa na Baba yake Mzazi  zaidi ya miaka 20.

 

Akizungumza na Huheso Digital Tv Amina Imamu Kibila ambaye ni Mama mzazi wa Binti huyo ameelezea kwa uchungu kuhusiana na changamoto  ambazo anazipitia binti yake ambapo baadhi ya ndugu zake wamemtenga  mama huyo wakiamini kuwa ameleta mkosi kwenye ukoo wao.

 

Mama mzazi wa binti huyo  ameeleza kuwa anapata changamoto kubwa ya kumhudumia  Binti yake maana yeye mwenyewe hana kipato chochote cha kukidhi mahitaji yake  na anaishi katika mazingira magumu ikiwemo kukosa  mahali pa kuishi.

 

Baadhi ya majirani wa eneo hilo  Monica Richard na  Sande Buluba wamezungumzia Maisha halisi ya Binti huyo  kuwa anapata shida sana maana hawezi kufanya kitu chochote  mfano kutembea, kuzungumza, kula, kufua, n.k

 

Kwa upande wake mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Ilindi  Ndg Dogo Mheziwa ametoa wito kwa jamii kuacha tabia ya kuwatenga watu wenye ulemavu na kuondokana na imani potofu kuwa ulemavu siyo mkosi bali ni mpango wa Mungu jamii inatakiwa  kuwajali na kuwapa nafasi


Ukiguswa na unahitaji kumsaidia tafadhali wasiliana na Mama Rehema kwa Namba 0753-367-865 na 0688-598-292.

Ukiitaji kumsaidia Rehema tafadhali namba zake hizo hapo juu pia unaweza kutuma Msaada wako kupitia akaunti 

0150059582900 - Huheso CRDB bank 


Pata muda uangalie masaibu anayopitia Rehema na Mama yake katika kumtunza baada ya kutelekezwa na Baba yake miaka 21 iliyopita.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments