AMUUA KAKA YAKE KWA PANGA WAKIGOMBANIA NYAMA YA UTUMBO

Polisi huko Murang'a nchini Kenya wanamsaka mwanaume wa miaka 30 anayeshukiwa kumuua kakake mkubwa kufuatia mzozo wa nyama ya utumbo ya KSh 50 sawa na shilingi 1000 ya Tanzania.

Katika kisa cha Jumapili, Septemba 18,2022 kilichotokea kijiji cha Ihumbu, mshukiwa alidaiwa kumkata marehemu, Moses Mwaura, kichwani kwa kutumia panga na kumwacha akiwa amepoteza maisha yake. 

Baba yao Onesmus Nduati aliwaambia polisi kwamba alisikia zogo katika boma lake na alipofika, akawapata wawili hao wakizozana kuhusu kitoweo hicho, Nation iliripoti. 

Nduati alisema mshukiwa huyo alieleza kuwa alinunua nyama hiyo katika duka la karibu na kuiweka kwenye shina la mti nyumbani kwao ili kujisaidia.

Hata hivyo, alipotoka nje alikuta matumbo hayapo kwa kuwa kakake mwenye umri wa miaka 36 ambaye alikuwa katika boma hilo alikuwa ameyaiba.

 Baba huyo alisema mtuhumiwa huyo ambaye kwa ujumla ni mgomvi hakutaka kusuluhisha mgogoro huo kwa amani na kumshambulia kaka yake kwa panga.

 “Huyo kijana ambaye kwa kawaida ni mgomvi na mwenye hasira kali hakutaka kusuluhisha mzozo huo kwa amani bali alimshambulia kakaake mwenye umri wa miaka 36 kwa panga,” alisema Nduati.

 Mwaura alikimbizwa katika hospitali ya Maragua Level Four ambapo ilitangazwa kwamba tayari alikuwa amekata roho njiani.

 Mwili wake ulipelekwa katika Hospitali ya Maragua Level Four ukisubiri uchunguzi wa maiti. Mshukiwa huyo kwa sasa yupo mafichoni na silaha ya mauaji.

Chanzo - Tuko News

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post