APIGWA HADI KUFA NA MMEWE KISA KACHELEWA KURUDI NYUMBANI AKITAFUTA MAREJESHO YA KIKOBA


Aisha Ramadhani (Marehemu)

Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma linamshikilia Peter Mwakiposile kwa tuhuma za kumuua mkewe Aisha Ramadhani mkazi wa Chidachi kwa kupigwa hadi kufa, kwa kosa la kuchelewa kurudi nyumbani akitafuta fedha za Marejesho la kikundi cha kikoba.


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma ACP Martin Otieno ameeleza kuwa mtuhumiwa yupo chini ya ulinzi wakati akisubiri taratibu za kufikishwa mahakamani huku mwili wa marehemu Aisha Ramadhani ukiwa umehifadhiwa chumba cha kuhifadhia maiti kwenye Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma kwa taratibu za mazishi.

Mama wa marehemu Aisha Ramadhani amesimulia kuwa alipigiwa simu na mkwe wake Peter Mwakiposile wakati akitekeleza unyama huo ambapo ilisikika sauti ya marehemu ikiomba msaada kitendo ambacho kilipuuzwa na mumewe huku watoto wa marehemu wakisema mama yao aliondoka nyumbani saa 12 jioni na kurudi saa 2 usiku baada ya kwenda kuomba fedha kwa rafiki yake kwa ajili ya rejesho ndipo baba yao akaanza kumpiga sehemu mbalimbali za mwili wake.

Chanzo - EATV

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post