AJALI YA HIACE ILIYOBEBA MAGAZETI YAUA NA KUJERUHI TANGA

Watu wawili wamefariki dunia na wengine watatu kujeruhiwa baada ya gari dogo aina ya Toyota hiace lililokuwa limebeba magazeti kuligonga kwa nyuma scania wakati dereva akijaribu kulipita alfajiri ya leo Septemba 7, 2022, katika eneo la Kwedizinga wilayani Handeni mkoani Tanga.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Tanga Safia Jongo, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo hii leo na kusema chanzo cha ajali hiyo ni dereva wa hiace Fransic Akwilini Masawe (36), kutaka kulipita gari lililokuwa mbele yake na hivyo kujikuta akiligonga lori.

"Ukiangalia ajali hii chanzo kikubwa ni dereva wa hiace ambaye alitaka kulipita gari lililopo mbele yake ndipo alipokutana na lori na kuligonga, hivyo nitoe wito kwa madereva kutiii sheria za usalama barabarani kuepukana na ajali ambazo zinaweza kuepukika" amesema RPC Jongo.

CHANZO -EATV

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post